Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, August 10, 2009

STARS YAENDA RWANDA!!!


Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ama The Blues of Africa imeagwa rasmi tayari kuelekea nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya taifa ya nchi hiyo.
wakati wakiagwa wamekabidhiwa bendera na Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya habari utamaduni na michezo, Charles Matoke na kuwataka kurudi na ushindi.
Wachezaji watakaosafiri na timu hiyo ni Shabani Dihile, Ali Mustapha, Juma Jabu, Erasto Nyoni, David Naftar, Stephano Mwasika, Shabani Nditi, Kelvin Yondani, Juma Nyoso, Mwinyi Kazimoto, Nurdin Bakari, Razack Khalfan, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Danny Mrwanda, Rashid Gumbo, Kigi Makasi, John Bocco, Zahoro Pazi na Salum Sued.
Shadrack Nsajigwa ameacha kutokana na kuwa majeruhi hivyo asingeweza kucheza katika mchezo huo lakini pia hayumo Musa Hassan 'Mgosi' katika kikosi hicho kutokana na kwenda Norway katika majaribio.
Imebainishwa pamoja ya kuwepo katika msafara huo mshambuliaji Tegete ataanzia benchi kwani alikuwa majeruhi lakini sasa ameanza kufanya mazoezi mepesi.
Naye kipa Shabani Kado anaweza kuchukua nafasi ya Dihile ambaye hali bado sio nzuri lakini amemweka katika msafara huo huku akimwangalia maendeleo ya afya yake.

No comments :

Post a Comment