Shirikisho la kandanda Tanzania limetupilia mbali maombi ya klabu ya Simba wachezaji wake kujiunga na kambi ya timu ya taifa hapo Agosti mara baada ya kumalizika kwa tamasha la Simba.
Frdrick Mwakalebela ni katibu mkuu wa TFF amesema mchezo wa Simba ni wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya klabu hiyo, Taifa Stars inajukumu la kitaifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda hapo Agosti 12 Mjini Kigali Rwanda.
Mwakalebela amesema katika jukumu hilo uzalendo haunabudi kuwekwa mbele hasa ikizingatiwa timu ya taifa imekuwa ikipata wachezaji toka katika vilabu vya Tanzania ikiwemo Simba.
Mwakalebela amesema anaamini Simba ni binaadamu na wanaelewa umuhimu wa Timu ya taifa pamoja na mchezo huo wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, hivyo anaamini wachezaji hao wataungana na wenzao kambini muda wowote kuanzia sasa.
Aidha Mwakalebela amesema wako tayari kuwaruhusu wachezaji wa Simba kuungana na wenzano wakati wa tamasha la Simba linalotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.
Amewataka wachezaji wa Simba kujiunga na wenzao katika kambi ya timu ya taifa haraka iwezekenavyoo.
BONDIA RAMADHANI MIGWENE AMUWEKEA MIKWALA ALBANO CLEMENT BAADA YA KUKIMBIWA
NA HABIBU PENGO
-
BONDIA RAMADHANI MIGWEDE baada ya kukimbiwa na mpinzani wake Habibu Pengo
aliesaini nae kuzipiga mara ya kwanza sasa amebadilishiwa mpinzani na
atacheza na...
2 years ago
No comments :
Post a Comment