Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 2, 2009

ROBERT SENTONGO AMALIZA MINONG`ONO AFRICAN LYON

Robert Sentongo (katikati) akiwa na viongozi wa African Lyon katika uwanja wa ndege wa kimataifa Mw. Julias Nyerere jijini Dar Es Salaam. Robert Sentongo alipokewa pia na kapteni Mohammed Abdallah (wa pili toka kulia).
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Robert Sentongo amemaliza minong`oni ya kwamba huenda akaingia mitini na fedha za African Lyon kama alivyofanya kwa klabu ya Simba miaka miwili iliyopita baada ya kuwasili tayari kuitumikia klabu hiyo.
Akizungumza baada ya kuwasili nchini Robert Sentongo amesema yuko hapa nchini kwa ajili ya kuichezea klabu ya African Lyon na kudai alihitaji ushawishi kabla ya kujiunga.
Ameishukuru klabu yake ya KCC kwa kumpa ruhusa kujiunga na Afrcan Lyon, viongozi wake pamoja na wachezaji laini amekiri ulikuwa umefika wakati wa kupiga hatua nyingine katika ulimwengu wa soka tofauti na nyumbani.
Amekiri kutambua kwamba African Lyon ni klabu ngeni katika ligi kuu Tanzania bara, lakini anatambua na mipango mikubwa ya mafanikio, na kudai anaamini African Lyon itamsaidia zaidi kupiga tambo katika soka na kutimiza ndoto zake za kutaka siku moja kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Sentongo licha ya kukataa kutaja dau lililomfanya kumwaga wino katika klabu hiyo, lakini anakadiriwa kuweka kibindoni kiasi cha Dola za Marekani 80,000 na kutajwa kuwa huenda akawa ameweka rekodi ya usajili msimu huu.

No comments :

Post a Comment