wa muziki wa kizazi kipya nchini Chid Benzi na Dully Sykes wanatarajia kusindikiza mpango wa Indiafrika wa kuunganisha historia ya Utamaduni kati ya Tanzania na India.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mbunifu wa mitindo nchini Mustapha Hasanali alisema mpango huo utahusisha vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo nchini na utafanyika kesho katika ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema pia mpango huo umeunganisha ushirikiano katika masuala ya mitindo kupitia mashindano ya Swahili Fashion Week ambayo yatatoa mshiriki mmoja atakayeiwakilisha nchi kwenye mashindano ya ubunifu ya India fashion week.
Naye Balozi wa India Pinak Chakravarty ambaye pia ni Katibu Maalumu wa idara ya Umma ya Wizara ya Mambo ya Nje na Diplomasia alisema mpango huo utakuza mbinu za ushirikiana wa kimaendeleo baina ya India na nchi za Afrika.
Chakravarty alisema India na Afrika
inaingia katika ukurasa mpya wa kihistoria kupitia ukoloni na unyonyaji wa kiuchumi hadi kufikia uhuru.
Alisema uhusiano wa Tanzania na nchi nyingine unazidi kukua kwa kasi na kwamba umeegemea zaidi katika uhusiano wa kiuchumi katika dunia ya utandawazi.
Alisema pia umejikita katika mpango maaalumu wa kibiashara ambao makao makuu yake yako mjini Delhi, na unasimamiwa na idara maalum ya Umma, chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya India.
Alisema mpango huo wa Indiafrika ulizinduliwa mwaka 2011 na kwamba mpango hup unakaribisha mbadilishano wa mawazo kati ya vijana kutoka Africa na India kupitia mfululizo wa mashindano mbalimbali ya wajasiriamali, ubunifu na vipaji mbalimbali kwa vijana.
Alisema pia ina lengo la kujenga jukwaa la vijana kutoka India na Afrika lenye nguvu, uvumbuzi na ushindani.
"Kuongezeka kwa uwezo wa ubunifu na kiutamaduni, ni muhimu kwa ajili ya mafanikio, na kuwajenga vijana kuwa raia wazuri wa kimataifa na kukuza ndoto na matarajio yao katika nchi yoyote duniani,"alisema.
Alisema mashindano hayo yatakuwa katika kategoria tatu ambapo kila kategoria washindi watatu watakabidhiwa dola 1000 kila mmoja kutoka kila kanda ambazo ni Afrika Mashariki, magharibi, ya Kati na kusini huku katika fainali itakayowakutanisha washindi wa kanda hizo mshindi atapata dola 10,000.
Alisema washindi hao watapewa ziara ya siku tano itakayoambatana na semina mikutano ya kibiashara itakayokuwa ikifanyika nchini India na katika nchi mbalimbali za Afrika
No comments :
Post a Comment