Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati) akimkabidhi jezi na pesa
taslimu kiongozi wa Klabu ya Michael’s Pub, Michael Bundala wakati wa
ufunguzi wa mashindano ya Safarli Lager Pool Taifa Mkoa wa Tanga jana.
Kushoto ni Meneja mauzo wa TBL Mkoa wa Tanga,Bahati Mbise.
**************************
Na Mwandishi Wetu,Tanga
MKUU
wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego ameahidi kutoa pesa taslimu 200,000
kwa timu itakayofanya vizuri katika mashindano ya 'Safari Lager Pool'
ngazi ya Mkoa wa Tanga ili kuweza kuipa hamasa ya kwenda kufanya vizuri
katika mashindano hayo ngazi ya taifa.
Dendego
alitoa wito huo juzi wakati wa Makabidhiano ya vifaa vya mashindano
hayo kutoka kwa Kampuni ya Bia nchini TBL kwa timu 9 ambazo zinashiriki
mashindano hayo ambayo yataanza ramsi kesho katika ukumbi wa Mangroose
iliyopo sahare jijini Tanga.
Alisema
mchezo huo ni kama michezo mengine hivyo aliwataka wadau wa mchezo huo
kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri ya kuuweka mchezo huo nje ya
mabaa ili uweze kupendwa na watu wa kila aina.
Aidha aliwaomba
viongozi wa mchezo huo kuwa wanapokaa kwenye kamati zao kuhakikisha
wanaweka muda maalumu wa kucheza na kueleza kuwa wanapaswa kuujengea
mtazamo mzuri ili uweze kupendwa zaidi.
Katika
makabidhiana hayo Kampuni ya Bia nchini (TBL)kupitia bia yake ya Safari
Lager walikabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh.Milion 5 kwa timu
zote tisa ambazo zinashiriki mashindano hayo ambao yataanza kesho na
yanatarajiwa kufikia tamati Jumapili wiki hii ambapo yatafanyika siku
nne.
Vifaa
vilivyo kabidhiwa ni pamoja na tisheti na pesa taslimu kwa kila timu
shiriki katika mashindano hayo ambavyo ni High Way,Spaider,Members
Family,Kijiti Pool Table,Tanga Beathing Club,Kibo Garden Pool,Maiko
Pub,Kange Brothers na Ngamiani Sports Club.
Akizungumza
wakati akikabidhi Vifaa hivyo Meneja Mauzo wa Kampuni ya TBL Mkoa wa
Tanga,Bahati Mbise alizitaka timu shiriki kuhakikisha zinatumia ipasavyo
vifaa hivyo na kuweza kucheza kwa ushindani na kuwa makini ili kuweza
kupata timu bora ambayo itawakilisha vema mkoa katika mashindano hayo
ngazi ya taifa.
|
No comments :
Post a Comment