Mheshimiwa Rais,kwa niaba ya Bodi,Kamati kuu,wanachama na wadau wa Shirikisho la Filamu Tanzania,TAFF,
napenda ufahamu kwamba Shirikisho ni taasisi inayoundwa na muungano wa
vyama vinavyojihusisha na kazi za utayarishaji wa filamu nchini, ambalo
lilianzishwa kwa tamko la serikali mwaka 2009 na kusajiliwa mwaka 2010
kwa sheria namba 23 ya mwaka 1984 lakini pia inatekeleza majukumu yake
kwa kupitia sheria namba 4 ya mawaka 1976 ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania na kanuni zake.
Mheshimiwa Rais, Vyama
vinavyounda Shirikisho hili ni Chama Cha Waigizaji, Chama Cha
Waongozaji, Chama Cha Watayarishaji, Chama Cha Wasambazaji,Chama Cha
Wahariri, Chama Cha Watafuta mandhari , Chama cha Watunzi na chama cha
Wapiga picha za filamu, vyama vyote vimesajiliwa na kutambulika kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Kwa kipindi kirefu sana tasnia ya filamu na sekta ya sanaa kwa ujumla imekuwa katika mazingira hatarishi kwa mustakabali wa maslahi ya wasanii wenyewe. Lakini tatizo hili lilisababishwa na
a. mtazamo hasi ambao ulianzia katika misingi mikuu ya sheria
kuifanya sanaa kuwa ni kiburudisho na
b. mfumo mbaya wa biashara ya sanaa ambapo bei haipangwi na
mtayarishaji bali hupangwa na mnunuzi.(Mfumo huu umesa
babisha kutowepo kwa takwimu sahihi za mapato yanayotokana
na shughuli za tasnia ya filamu na filamu zenye ubora
viwango vya soko la kimataifa )
jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa sanaa ya Tanzania kudumaa,kuwa watumwa katika kazi zao na wasanii kutokuwa na maslahi stahiki yanayotokana na kazi zao.
No comments :
Post a Comment