MWENYEKITI WA TAMASHA LA FIESTA 2012 SEBASTIAN MAGANGA AKIZUNGUMZA LEO MCHANA KATIKA UZINDUZI RASMI ULIFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.
WATANGAZAJI MAARUFU WA REDIO CLOUDS WAKIWA MZIGONI MILLAD AYO NA BARBARA HASSAN
WADAU MBALIMBALI WAKIFUATILIA UZINDUZI HUO ULIOFANYIKA LEO MCHANA.
MILLAD AYO AKIMHOJI JAMBO MWIMBAJI WA MUZIKI WA KIZAZI CHA SASA MWASITI ALMASI .
ZAWADI ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILLIONI MIA HAMSINI ZITAWEZA KUTOKA KWA MASHABIKI NA WAPENZI WA FIESTA, YAKIWEMO
1: MAGARI AINA YA TOYOTA VITZ SITA KUTOLEWA KILA MMOJA IKIWA NA THAMANI YA SHILINGI MILLIONI NANE.
2: PIKI-‐PIKI (BODA-‐BODA) KUMI NA NNE KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA SHILINGI MILLIONI MOJA NA NUSU
3: SIMU 50 ZA BLACKBERRY KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA SHILINGI LAKI SABA.
4: NOKIA DABO-‐DABO ZENYE TOCHI MIA HAMSINI NA LAINI MBILI ZENYE THAMANI YA SHILINGI 80,000 KILA MOJA.
5: ZAWADI MBALIMBALI KUTOKA SERENGETI PREIMIUM LAGER NA CLOUDS MEDIA GROUP ZIKIWA NI PAMOJA NA TSHIRTS, BEER ZA SERENGETI PREIMIUM LAGER TIKETI ZA BURE NA FEDHA TASLIMU KWA PAMOJA VYOTE VIKIWA NA THAMANI YA SHILINGI MILLIONI20.
PRIMETIME PROMOTIONS,CLOUDS MEDIA GROUP NA MDHAMINI MKUU SERENGETI BREWERIES LIMITED KUPITIA BIA YAO SERENGETI PREMIUM LAGER; KWA KUSHIRIKIANA NA GAPCO TANZANIA LIMITED NA PUSH MOBILE, WANAYOFURAHA KUBWA KUKULETEA SERENGETI FIESTA 2012, IKIWA NI MAADHIMISHO YA MIAKA 11 WA TAMASHA HILI.
SERENGETI FIESTA NI MSIMU MAHKSUSI KWA AJILI YA WAPENZI NA WADAU WOTE WA MUZIKI, UTAMADUNI, NA BURUDANI AMBAPO KWA KARIBU MWEZI MIWILI WATANZANIA KWENYE MIJI ZAIDI YA KUMI NA MBILI KUZUNGUKA NCHI HII, WATAWEZA KUENDELEZA MSIMU WAO WA DHAHABU KWA KUSHUHUDIA JUKWAA LENYE UWELEDI NA MVUTO KUTOKANA NA BURUDANI HADHARA YA WASANII MBALIMBALI WANAOCHIPUKIA NA WENYE MAJINA NA UMAARUFU MKUBWA,
SERENGETI FIESTA 2012 ITAANZA KWA SHUGULI NA MASHINDANO YA AWALI KUANZIA TAREHE 30 JUNE HADI TAREHE 17 JULAI MWAKA HUU NA KUFUATIWA NA TAMASHA LENYEWE KATIKA MIJI MBALIMBALI TANZANIA, IKIWEMO TABORA NA SINGIDA KWA MARA YA KWANZA, AMBAPO SERENGETI FIESTA INATARAJIWA KUANZIA MJINI MOSHI, MKOANI KILIMANJARO TAREHE 24 AGOSTI NA KUENDELEA KATIKA MIJI MINGINE HADI TAREHE 6 SEPTEMBA 2012, KILELE KIKIWA NI JIJINI DAR-‐ES-‐SALAAM.
KAULI MBIU YA SERENGETI FIESTA 2011 NI “MUONEKANO MPYA-‐BURUDANI ILE ILE...BAAAAS”, HII INATOKANA NA KWAMBA SERENGETI FIESTA IMEWEZA KUWA SEHEMU MUHIMU YA BURUDANI KATIKA MAISHA YA VIJANA WA KITANZANIA KWA MIAKA KUMI YA UHAI WAKE, HIVYO MWAKA WA 11 KAMATI KUU YA MAANDALIZI YA SERENGTI FIESTA IMEDHAMIRIA KUONGEZA UFANISI WAKE KWA KUHUSISHA MAMBO MAPYA YENYE KULETA TIJA KWA WAPENZI NA WAFUATILIAJI WA SERENGETI FIESTA 2012.
No comments :
Post a Comment