Msanii
wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akikimbilia basi la Magereza
mara baada ya kutoka kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili kwenye
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.
KESI
inayo mkabili msanii kinda wa Filam nchini Elizabeth Michael (Lulu)
imezidi kuwagawa wanasheria baada ya mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam
kushindwa kusikiliza Shauri la Umri wa msanii huyo, kutokana na madai
yaliyowasilishwa na wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda.
Kaganda
alidai kuwa wamekata rufaa mahakama ya rufaa kupinga mahakama kuu
kusikiliza shauri hilo kutokana na mahakama ya Kisutu kufanya makosa ya
kulipeleka shauri hilo mahakama kuu ambayo haina haki ya kusikiliza
shauri hilo na kutaka lirudishwe tena mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mawakili
wanaomtetea msanii huyo walipinga vikali kauli hiyo nakudai haikufuata
taratibu za kisheria kwa sababu siku ya leo ilikua ni siku ya
kusikiliza shauri kuhusu umri na sio kuleta pingamizi hilo, pamoja na
hilo jaji anaesikiliza kesi hiyo hana taarifa zozote kuhusiana na jambo
hilo na kulifanya likose uhalali wa kukubalika.
Hata
hivyo jaji Mkuu anae sikiliza Shauri hiolo Dk.Twalibu Fauzi, alikataa
katakata maelezo ya wakili wa upande wa Serikali nakusema suala hilo
aliwezi kurudishwa tena Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu na kutoa kauli
kwamba Mahakama Kuu itaanza kusikiliza kesi hiyo July 9 mwaka huu. Lulu
amerejeshwa Rumande kuendelea kusubiri hatima ya maamuzi ya kisheria.
No comments :
Post a Comment