Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, June 19, 2012

KAMPUNI YA SAMSUNG TANZANIA YAGAWA SIMU 200 BURE.



Wateja wakiwa katika foleni ya kununua simu aina ya Galaxy Pocket katika duka la wakala wa Samsung Tanzania jijini Dar es Salaam ambapo wateja 20 wa mwanzo kila mmoja alipata simu za bure
 
KAMPUNI ya Samsung Tanzania jana imegawa simu 200 bure aina ya Galaxy Pocket kwa wateja wa kwanza kununua simu hizo.
Promosheni hiyo ya siku moja imekuja baada ya kampuni hiyo kuzindua simu hizo Juni 14 mwaka huu.
Akizungumza jijini  Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuanza kuuzwa simu hizo na kutolewa bure, Meneja Mauzo na Usambazaji Kitengo cha Samsung Mobile Sylvester Manyara alisema promosheni hiyo iliyoendeshwa nchi nzima ilitangazwa kupitia redio na  mitandao mbalimbali ya kijamii.
Alisema kupitia facebook waliwataka wateja wajitokeze kununu simu hizo katika maduka ya Samsung ili wapate moja bure, kwasababu ni promosheni ya siku moja.
“Hii promosheni ilikuwa ni kwa ajili ya wateja 200 tu … kwa maana tumetoa simu 400; yaani 200 za bure na 200 za kununua,”alisema Manyara huku akiwashauri Watanzania wanunue bidhaa mbalimbali za Samsung.
Naye Frank Wada mkazi wa Dar es Salaam, aliyenufaika na promosheni hiyo alisema amefarijika kununua simu hiyo na kupata nyingine bure.
“Unajua kila duka lilikuwa linapokea wateja 20; nilikwenda duka la kwanza nikakuta kumejaa nikaambiwa waliokuwepo wanatosha  ndio nikaja hapa na kupata bahati hii,”alisema Wada huku akicheka.

No comments :

Post a Comment