TUZO YA DHAHABU YA NDOVU
Mpishi Mkuu wa Kampuni ya bia Tanzania TBL Gaudence Mkolwa, akipokea tuzo ya kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award”kutoka kwa Meneja wa bia ya Ndovu Special Mult Pamela Kikuli, baada ya kukabidhiwa na Meneja
wa Wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi
Kulwa (kulia), jijini Dar es Salaam kushoto ni Meneja wa habari na
mawasiliano Edith Mushi.
Grand Gold Award
Meneja wa Wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa, akikabidhi tuzo
ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa kimataifa
ijulikanayo kama “Grand Gold Award” kwa Meneja wa bia ya Ndovu Special
Mult Pamela Kikuli, baada ya kinywaji hicho kinachozalishwa na kampuni
ya bia Tanzania TBL, kupata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo.
MENEJA wa
wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa,
amesema kampuni yao inajiskia faraja sana kufanya kazi na kampuni ya bia
Tanzania TBL kutokana na mafanikio wanayo ya pata kimataifa..(Picha na
Intellectuals Communications Ltd)
Akikabidhi
tuzo tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa
kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award” Kulwa amesema kampuni yao
ina mtandao wa vituo 35 ikiwemo Tanzania hivyo wanahakikisha kufikisha
huduma zao kwa wakati kwenye vituo vyote ili kwenda sawa na wateja wao.
Awali akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema;
“Tunayo
furaha kubwa sana kuwajulisha wadau wa Bia hii ya Ndovu Special Malt
juu ya ushindi huu mkubwa ambao Bia hii imenyakua katika tuzo za bidhaa
za kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa
bidhaa ya “Monde Selection International Quality Institute” iliyopo
Athens, Ugiriki. Tuzo hii yenye hadhi ya juu kabisa katika ubora wa
bidhaa kimataifa inajulikana kama“Grand Gold Award” na hushindanisha bidhaa toka Mataifa mbalimbali ambapo mwezi huu Aprili taasisi hiyo imetangaza rasmi kuwa “Ndovu Special Malt”imeshinda tena tuzo ya “Grand Gold” kwa mwaka 2012. Alisema Pamela.
No comments :
Post a Comment