Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi
Mcheza sinema toka Marekani
Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt.
Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na
ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt.
Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita
kila mwaka.
Ujio wa Lorenz ambaye amecheza
sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight
umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake
umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.
Akizungumza na waandishi wa
habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa
ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana
furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu
duniani uko Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog
na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi
kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye
ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz
alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya
kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.
“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho
yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na
sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York
City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital)
la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages
iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya
Manispaa ya Uhuru Park.
Mji wa Moshi na viunga vyake
vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani ambao wamekuja
kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa kuitangaza
Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa
na Marie Frances mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania wa
Tanzania nchini Misri.
Mbio hizi zimejijengea umaarufu
mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na
Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa
limezipa nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa duniani wakati
jarida la Forbes la Marekani lenye wasomaji wengi duniani limeipa
nafasi ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya Moshi itampa barabara na kuiita
“Marie Frances Boulevard”mwaka 2009.
Mbio hizi hukimbiwa na watalii wa
Warekani wanaokuja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea
mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro Marathon zinajulikana kama 7
continental races zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya dunia.
Ratiba ya Deidre Lorenz
inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto yatima cha
Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na
watoto hao na kuwasomea hadithi mbalimbali za watoto zilizoandikwa na
Waltz Disney mwandishi maarufu wa karne ya ishirini wa Marekani.
Siku ya jumamosi atatembelea
hospitali ya KCMC ambapo atakutana na manesi ili kuwapa shavu kwa kazi
yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya jumamosi atahudhuria Pasta Party
ambapo atapata nafasi ya kukutana na wakimbiaji wengine na kuchagua
namba ya kukimbia kesho yake siku ya jumapili tarehe 24 juni.
No comments :
Post a Comment