Miss Utalii Tanzania, tofauti na mashndano mengine
ya urembo, ni zaidi ya shindano la urembo, kwani linalenga katika
kutangaza na kuhamasisha Utalii,Utamaduni, Mianya ya
Uwekezaji,Elimu,Afya ya Jamii,Utalii wa ndani,Utalii wa
kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikitano Kitaifa na kimataifa.
Shindano hili pia linahamasisha vita dhidi ya Umasikini,Iharibifu wa
mazingira,uwindaji haramu,Uvuvi Haramu,Ujinga,Maradhi, Tamaduni kongwe
na Potofu. Miss Utalii Tanzania pamoja na uchanga wake, tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2005, ni shindano lenye mafanikio makubwa kuliko shindano
jingine lolote nchini kitaifa na kimataifa kwani pamoja na kuipa heshima
Tanzania ya kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la Miss Tourism World
2006, shindano hili ndilo lililo andika historia ya Tanzania kutwaa taji
la kwanza la Dunia kabla na baada ya uhuru, pale tulipo twaa taji la
Miss Tourism World 2006, pia shindano hili ndilo pekee nchini
linashikilia rekodi ya kutwaa mataji ya dunia katika kila shindano
tulilo shiriki,tumetwaa mataji 6 ya dunia tangu 2005. Kutokana na
mafanikio haya , Tumepewa heshima ya kuaandaa shindano la Dunia la Miss
Umoja wa Mataifa mwaka 2013 hapa Tanzania. Ni shindano pekee nchini
ambalo washiriki wake hawavai mavazi ya kuogelea, bali mavazi ya heshima
yasiyo mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yaliyo buniwa na kushonwa
kwa malighafi za tanzania tu.
Link yetu ni : http://www. misstourismorganisation. blogspot.com
Facebook Page: https://www.facebook.com/ MissUtaliiTanzania
E-Mail: missutaliitanzania@gmail.com
No comments :
Post a Comment