Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Waandishi wa Habari Tanzania (TAJONET) wakiwa katika uzinduzi wa mtandao huo.
Mjumbe wa Kamati ya TAJONET, Neema Mgonja akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Wanachama wa Mtandao huo.
Zaituni Kibwana (kushoto) akiwa na mdau
Mwenyekiti
wa muda wa Mtandao wa Waandishi wa Habari Tanzania (TAJONET), William
Shao akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mtandao huo uliofanyika
jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Katibu wa Mtandao huo, Eben-Ezery
Mende.
Chalila Kibuda akizungumza katika uzinduzi wa Mtandao huo.
WAANDISHI wa
habari wamekutana jijini Dar es Salaam na kuanza mchakato wa kuunda
mtandao utakaoweza kusimamia, kupigania na kutetea haki zao.
Akizungumza
katika kikao hicho, Katibu wa muda, Ebenezer Mende, alisema kuwa mtandao
huo utajulikana kwa jina la ‘Waandishi wa Habari Tanzania (TAJONET) na
utakuwa wa nchi nzima.
Alisema mtandao
huo utatumika kama chachu ya kusaidiana katika matatizo mbalimbali,
ukiwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao na utahusika moja kwa
moja katika kusimamia maadili ya tasnia ya habari.
Mende
alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wandishi wa habari kujikuta
wakikabiliwa na matatizo mbalimbali huku wakikosa msaada.
Aidha
alibainisha kuwa TAJONET utakuwa bega kwa bega katika kuangalia suala
zima la afya ya wanachama kwa kuanzia ngazi ya chini kama matibabu awapo
hospitalini pamoja na misiba.
“Watu
wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ni kifo, bila kuangalia mambo
mengine kama ugonjwa, sisi hatutaki kujielekeza hivyo bali tunataka
tatizo la ugonjwa lipewe kipaumbele ili kuepusha vifo visivyo na
ulazima,” alisema Mende.
Alibainisha kuwa
mkutano huo umeteua viongozi wa muda 14, ambao kati yao wataunda
kamati ya rasimu ya upatikanaji wa katiba ya mtandao huo.
No comments :
Post a Comment