Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, June 27, 2012

BONANZA LA NANE NANE KURINDIMA KAWE



Salum Suleiman 'Sule Junior'

Mwandishi Wetu
Bonanza kubwa la mchezo wa mpira wa miguu linaloitwa 'Nane nane soccer bonanza' linatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es Salaam siku ya kilele cha sherehe za nane nane.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kampuni ya SULE'S INC. & ENTERTAINMENT, Salum Suleiman ambao ndiyo wadhamini wa Bonanza hilo timu mbalimbali kutoka katika maeneo ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam zitashiriki. 
"Maandalizi ya bonanza hili yameshafikia katika hatua nzuri kabisa, Kamati imefanya kazi nzuri mpaka kufikia hapa na tunategemea bonanza hili litafanyika kwa mafanikio makubwa,"alisema Suleiman.
Akizungumzia timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo, Suleiman alisema,"tunatarajia kuwa na timu nane ambazo zitachuana katika kuwania kombe siku hiyo na mashindano yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano."
Alisema wameamua kuliendesha bonanza hilo kwa mtindo wa mtoano ili timu ziweze kutoa ushindani wa kutosha na kuburudisha watu watakaojitokeza katika bonanza hilo.
"Washindi watapata zawadi, kwa sababu mshindi wa kwanza atatwaa kombe, mshindi wa pili pia atapata zawadi, mchezaji bora, mfungaji bora, kipa bora na mchezaji mwenye nidhamu wote hao watapata zawadi."
Sherehe za nane hufanyika kila mwaka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni siku ya kuadhimisha siku ya wakulima.

No comments :

Post a Comment