Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia)
akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa
kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone
5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel
kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha
internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo
(kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya
Apple.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa
kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone
5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel
kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha
internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo
( wa pili kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa
kampuni ya Apple.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
·Ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano nchini kuingia mkataba wa ushirikiano na Apple.
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma bora na nafuu leo
imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi
ya Apple.Airtel
imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano nchini
Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa simu huo jijini Dar es Saalam Meneja Masoko wa
Airtel Bi Prisca Tembo alisema” leo tunazindua simu ya iPhone 5s na
kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi ,
ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata
kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa
mwezi. Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kutumbelea maduka yetu
na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi, Beatrice Singano alisema
“Uzinduzi huu leo utato fulsa kwa wateja wetu kupata uzoefu tofauti wa
huduma zetu na kuwawezesha kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH
on, huduma ambayo imezinduliwa ili kuwawezesha wateja wetu kupata
internet yenye kasi zaidi bila kikomo kupitia mtandao wa Airtel”
“Simu hii ya iPhone 5s itawawezesha wateja wetu pia kupiga picha, kutuma video na kuwaunganisha na marafiki na familia . Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ofa hii ya simu ya iPhone 5s tembelea tovuti yawww.apple.com/phone “aliongeza mmbando.
No comments :
Post a Comment