Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila akijaribu
kusukuma moja kati ya viti 33 vilivyotolewa na asasi ya MUVIMA kwa ajili
ya hospitali ya wilaya ya Mufindi. Anayefurahi katikati ni mkurugenzi
mwenza wa MUVIMA, Albert Chalamila akipongezwa na Katibu wa Afya wa
Wilaya hiyo, Atupekisye Mwakifamba
Albert
Chalamila na baadhi ya wanahabari wakiangalia hali ilivyo ndani ya wodi
ya wazazi ya hospitali hiyo; hapa wanaonekana baadhi ya wajawazito
wanaolala chini kutokana na ukosefu wa vitanda
Na Denis Mlowe,Mufindi
ASASI
ya Mufindi Vijana kwa Maendeleo (MUVIMA) imetoa msaada kwa hospitali ya wilaya
ya Mufindi yenye matatizo mbalimbali kwa lengo la kusaidia kutoa huduma
bora kwa kutoa viti 33 vya kubeba wagonjwa.
Akikabidhi
msaada huo hivi karibuni Kaimu Mkurugenzi wa MUVIMA, Albert Chalamila alisema
asasi yao imeguswa na kero mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na kwa
kuanzia ililazimika kutafuta viti hivyo kwa lengo la kusaidia hospitali hiyo
yenye matatizo mbalimbali yanayofifisha utoaji wa huduma bora za afya,
zikiwemo zile za wajawazito na watoto,
Alisema
kwa msaada wa asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia
waliomba msaada huo baada kuomba msaada wa vitanda kwa ajili ya hospitali hiyo
hivyo vitanda 23 vimekwishawasili bandari ya Dar es Salaam na tumeanza na viti
vya kubeba wagonjwa.
Alisema
Mkurugenzi Mkuu wa MUVIMA, Cosato Chumi anaendelea na utaratibu wa kuvitoa
vitanda hivyo bandarini na mara baada ya shughuli hiyo kukamilika
vitakavifdhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo.
Kaimu Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila kwamba vitapunguza adha waliyokuwa wanapata watoa huduma wa hospitali hiyo ya kupokea na kubeba mikononi, wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.
Akishukuru
kwa msaada huo, Dk Mlimbila alisema hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa vifaa
tiba na dawa na akalitaja eneo lenye tatizo zaidi kuwa ni lile la huduma kwa
mjamzito na watoto.
Alisema
katika kuboresha huduma za uzazi, jengo lenye uwezo wa kulaza wajawazito zaidi
ya 100 na lenye chumba cha upasuaji na kile cha kuhifadhia watoto wanaozaliwa
kabla ya muda lilijengwa katika hospitali hiyo ambayo awali ilikuwa ikitumia
jengo lenye uwezo wa kuweka vitanda 27 tu.
Alisema
msaada uliotolewa na MUVIMA una umuhimu mkubwa katika hospitali hiyo kwani utarahisisha
huduma za ubebaji wagonjwa kutoka eneo moja hadi lingine na utapunguza idadi ya
wajawazito wanaolala chini baada ya vitanda vilivyoahidiwa kuwasili.
Naye
Katibu wa Afya wa wilaya hiyo, Atupakisye Mwakifamba aliwataka MUVIMA na wadau
wengi kujitokeza kuzimaliza kero za utoaji huduma zinazoikabili hospitali hiyo
na vituo vingine vingi vya huduma wilayani humo.
Mwakifamba
alisema pamoja na wilaya hiyo kuwa na idadi ya kuridhisha ya watoa huduma wenye
ujuzi, inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa tiba, dawa na magari ya kubeba
wagonjwa.
No comments :
Post a Comment