Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77 na
China, uliofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia jana Juni 15, 2014.
Sehemu ya washiriki na wawakilishi wa viongozi wa mataifa mbalimbali katika mkutano huo.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
HAKIKISHENI TUNAKUWA NA CHAKULA CHA KUTOSHA DKT. BILAL AWAAMBIA G77+CHINA
Na Mwandishi Maalum, St Cruz Bolivia
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amezitaka nchi wanachama wa G77+China, kuhakikisha zinaboresha kilimo
ili ziwe na hifadhi ya kutosha ya chakula kwa wananchi wake.
Akihutubia
mkutano wa mwaka kwa nchi za G77+China ambao pia ni kilele cha
maadhimisho ya miaka 50 ya umoja wa nchi hizi, unaofanyika jijini St
Cruz De Sierra, Dkt Bilal alisema nchi za umoja huu zina maeneo mazuri
kwa kilimo na hivyo ni muhimu kuyatumia maeneo haya katika kuzalisha
chakula kwa lengo la kuhifadhi na kuwa na usalama wa chakula nyakati
zote.
Dkt.
Bilal alisema, nchi hizi kwa pamoja zinahitaji kuwa na kauli moja
kuhusu masharti yanayowekwa na nchi kubwa hasa katika kilimo na kuelezea
kuwa ili mafaniio makubwa yapatikane, lazima uwepo uwekezaji wa ndani
katika kilimo sambamba na serikali za nchi hizi kuchangia shughuli za
uzalishaji ili kuwa na kilimo chenye tija kwa wakulima na kinachoweza
kuchangia usalama wa chakula.
Kuhusu
suala la mazingira, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wajumbe wa
G77+China kuwa, maazimio yaliyofikiwa Rio+20 na mapendekezo kuhusu
‘Kesho tunayoitaka’ yanazihitaji nchi hizi kupaza sauti zake kwa pamoja
kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani suala hili kwa sasa
haliwezi kutatuliwa na nchi moja bali linahitaji nguvu ya kila mtu
duniani.
Makamu wa Rais alifafanua kuwa bila kuwa na mazingira bora maendeleo endelevu yatabakia ndoto na pia kufanikisha Malengo ya Milenia kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa itakuwa vigumu kama suala la mazingira litaachwa kwa kila nchi kufanya inavyotaka.
“Kundi
hili lina kazi kubwa iliyo mbele yetu na hasa kuhusu malengo mapya ya
maendeleo baada ya kukamilika kwa muda wa Malengo ya Milenia mwakani.
Tunahitajika kubuni njia za kuzipatia nchi zetu maendeleo katika Nyanja
za uchumi, kijamii na mazingira ili tufanikiwe vema,” alisema Mheshimiwa
Makamu wa Rais.
Katika
hotuba hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alizungumzia kuhusu umuhimu
wa nchi hizi kuweka msisitizo wa kuwapa wananchi maji safi na salama,
umuhimu wa kuwa na nishati inayotosheleza matumizi ya uzalishaji, uwepo
wa huduma bora za afya na elimu ili kupiga hatua kwa haraka baina ya
wananchi wa nchi hizi. “Nafahamu kufanikisha haya yote ni kazi kubwa
lakini hatuna muda wa kusubiri. Ni lazima tufanye kazi ili kubadili hali
iliyopo,”alifafanua.
Mkutano
huo ambao umekamilika jana kwa mwenyeji wake Rais Evo Morales
kuwashukuru wanachama wa G77+China walioweza kushiriki mkutano huo, pia
ulionesha nia kwa wanachama wa nchi hizi kutafuta majibu ya changamoto
ya ukosefu wa ajira unaokabili wananchi wengi wa nchi hizi.
Viongozi wengi walisisitiza kuwa, suala la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kutazamwa upya na hasa ukizingatia rasilimali zilizopo katika nchi za G77+China ili zitumike katia kutengeneza ajira mpya zitakazoweeza kusaidia kuboresha maisha ya watu wa nchi hizi kwa miaka mingi ijayo.
Viongozi wengi walisisitiza kuwa, suala la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kutazamwa upya na hasa ukizingatia rasilimali zilizopo katika nchi za G77+China ili zitumike katia kutengeneza ajira mpya zitakazoweeza kusaidia kuboresha maisha ya watu wa nchi hizi kwa miaka mingi ijayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(wa pili kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wenzake waliohudhuria na kuzungumza katika mkutano huo wa
sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77 na China uliofanyika
jana Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati
wa ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika juzi usiku Juni 14,
jijini Santa Cruz, Bolivia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati
wa ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika juzi usiku Juni 14,
jijini Santa Cruz, Bolivia.
No comments :
Post a Comment