Moses Iriria, kutoka ANSAF (Mtafiti) akiwasilisha mada katika mjadala huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria akiwasilisha mada wa washiriki.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Matandao, Bi. Usu Mallya akiendesha majadiliano kwa washiriki.
Ofisa Miradi wa TAWJA, Asha Komba ikiwasilisha mada yake katika mjadala wa wazi. Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi. Sehemu ya washiriki wa mjadala huo wa wazi. Pichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai.
Pichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai
Mwanaharakati Badi Darusi akiwasilisha mada yake. Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MTANDAO
wa Jinsia nchini (TGNP Mtandao) umefanya mjadala wa wazi ulioshirikisha
taasisi mbalimbali zisizo za Serikali (NGO's) pamoja na wadau wa
masuala ya kijinsia juu ya uboreshaji wa uwajibikaji kwa kuzingatia
mgawanyo wa rasilimali kijinsia kwa huduma bora za kijamii nchini
Tanzania.
Mjadala
huo wa wazi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Blue
Pearl, pamoja na mambo mengine lengo kuu ilikuwa ni kuimarisha sauti ya
pamoja kudai uwajibikaji kwa watunga sera kwa kuzingatia mgawanyo wa
rasilimali kijinsia, kupiga vita rushwa na kuboresha utoaji huduma za
kijamii.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mjadala huo,
Kaimu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa TGNP Mtandao, Bi. Kenny Ngomuo
alisema malengo mahususi ya mjadala ni pamoja na kukuza uelewa wa
muktadha wa kimataifa, kitaifa na kijamii na athari zake kwa maisha ya
wanawake walioko pembezoni.
Alisema
lengo lingine ni kwa washiriki kubadilishana uzoefu na mafanikio ya
harakati mbalimbali kuhusu uchambuzi wa bajeti na ufuatiliaji wa
utendaji katika ngazi za jamii hadi taifa na pia kuweka mikakati ya
kuendeleza mapambano zidi ya rushwa, kukuza utawala bora ili kuboresha
utoaji wa huduma kwa jamii.
"...Malengo
mengine mahususi kwa washiriki wa mjadala huu ilikuwa kuweka kumbukumbu
za mafanikio yanayohusiana na mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni pamoja
na kupigania bajeti ya kijinsia na ufuatiliaji. Kuimarisha mitandao na
ujenzi wa nguvu za pamoja juu ya masuala ya bajeti ya kijinsia, vita
dhidi ya rushwa na huduma bora kwa jamii," alisema Bi. Ngomuo.
Kabla
ya kuanza kwa mjadala huo mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa washiriki,
ambazo ziligusa maeneo anuai ya huduma za kijamii, rushwa na changamoto
nyingine zinazoikabili jamii kabla ya wajumbe kupata fursa ya
kujadiliana kwa pamoja. Takribani washiriki 130 kutoka Dar es Salaam na
mikoa ya jirani ikiwemo Morogoro na Pwani wameshiriki mjadala huo.
No comments :
Post a Comment