Pichani
(kulia) ni Winga wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Simon Msuva, akimtoka
beki wa Zimbabwe, wakati wa mchezo huo uliopigwa jana, jijini Harare.
**************************************
TIMU
ya Taifa Taifa Stars, jana imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya
kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2015) baada ya
kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zimbabwe.
Kwa
matokeo hayo sasa Stars imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 kutokana
na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kutinga katika hatua ya pili sasa Stars inatarajia kukutana na
Msumbiji wiki mbili zijazo ambapo ikifanikiwa kupita hatua hiyo itaingia
katika hatua ya makundi.
Mabao
yaliyoiwezesha Stars kusonga mbele katika mchezo wa jana yalifungwa na
Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 26, na
Thomas Ulimwengu katika dakika ya 46, huku mabao ya wenyeji yakifungwa
na Danny Phiri katika dakika ya 13 na Willad Katsande katika dakika ya
55.
Baada
ya kumalizika dakika 90 za mchezo huo, Mwamuzi aliongeza dakika saba,
lakini bado hali ilionekana kuzidi kuwa ngumu kwa wenyeji waliokuwa
wakitafuta bao la kuongoza ili angalau kujaribu kujitetea kwa matuta.
Katika
mchezo ujao unaoikabiri Stars, iwapo Msumbiji wakitolewa Stars itatinga
moja kwa moja katika kundi F lenye timu za Zambia, Cape Verde na
Nigeria.
Wachezaji wa Taifa Stars wakijipa morali ya ushindi kabla ya kuanza kwa mtanange huo dhidi ya Zimbabwe jana.
Sehemu ya mashabiki wa Taifa Stars walioambatana na timu na baadhi ya Watanzania waishio Harare, wakishangilia kuisapoti Taifa Stars jana.
Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka beki wa Zimbabwe.
No comments :
Post a Comment