HABARI
za leo wasomaji wangu? Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa
shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku
hii.Mada leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila
kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.
Nimeamua
kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji
mimba na kutupa watoto na hata kuwa na watoto wa mitaani
yanasababishwa zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa.
Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.
Ni
muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo
iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi
nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35.
Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi.
Ili
kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku
ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi
ya mwezi unaofuata. Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 Oktoba
basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.
Kwa
mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika
mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya
16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua
mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini
akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni kwa sababu mbegu
za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi
48
baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai
likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo
zitarutubishwa.Chanzo GPL
No comments :
Post a Comment