NI Warembo waliongia kambini katika Hotel ya Ihesa iliyopo mjini Kahama tayari kuwania taji la Redds Miss Shinyanga 2014. |
NI Warembo waliongia kambini katika Hotel ya Ihesa iliyopo mjini Kahama tayari kuwania taji la Redds Miss Shinyanga 2014. |
Katika poz. |
Kama kawaida mambo ya mitembeo yao. |
NI Warembo waliongia kambini katika Hotel ya Ihesa iliyopo mjini Kahama tayari kuwania taji la Redds Miss Shinyanga 2014 wakionyesha dance. |
Hapo vipi....!! |
SHINYANGA KUMPATA MISS REDD’S 2014, JUNI 28.
MKOA wa Shinyanga unatarajia kumpata Mrembo wake “Miss Redd’s Shinyanga
2014”katika Kinyang’anyiro kitakachofanyika Juni 28,mwaka huu baada ya
Walimbwende 20 wenye haiba kuingia kambini katika Ukumbi wa Ihesa Hotel
&Resort Ltd ya mjini Kahama.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Asela Promotion inayoratibu wa
shindano hilo Asela Magaka alisema tayari maandalizi ya awali yameanza
ambayo ni kuwaweka kambini jumla ya warembo 20. ,kujifua ili kutwaa taji
hilo.
Alisema warembo hao wamepatikana kutoka
katika michuano ya urembo kutoka Wilaya sita za Mkoa wa Shinyanga ambazo
ni Kishapu, Kahama, Shinyanga Mjini, Msalala Shinyanga Vijijini na
Ushetu,huku wakiwa na mvuto mkubwa na viwango vinavyofafana hali ambayo
italeta ushindani mkubwa miongoni mwao.
Magaka alisema kuwa mashindano hayo
yanatarajia kufanyika tarehe 28/6/2014 katika ukumbwa Kisasa maarufu na
mpya wa Shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) Mjini Kahama na kuwataka
mashabiki na wapenzi kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani anatwaa taji
laMrembo wa Mkoa wa Shinyanga.
Mratibu huyo alisema kuwa katika shindano
hilo linatarajiwa kupambwa na Wasanii kutoka ndani na nje ya nchi
wakiongozwa na mfalme wa Taarabu Nchini Mzee Yusuph, Amani kutoka Kenya
na Mo Music.
Aidha
aliwataja wadhamini wa Shindano hilo kuwa ni SSCN TV ya Mjini Kahama,
Nonema Investiment, Trixie Social Media Market, Nyamizi Secretarial
Service, Royal Supermarket, NSSF, Coca Cola, Redds na Global Publisher.
Wengine
ni pamoja na Clouds FM, Three Jays’s Inverstment, CXC Africa,
Williamson Diamond, Saluti, Ihesa Hotel, Kahama Commonity Health
Dispensary, Tulliz Fashion, Ngeleja Gold Mine, Kahama Motel, Charitk
Pub, Glory Pads na Barrick Buzwagi.
Mratibu
huyo pia alisema kiingilio katika shindano hilo kinatarajiwa kuwa
shilingi 60,000 kwa watu wa jukwaa maalumu ( VIP) wakati shilingi 20,000
kitakuwa ni kwa watu wa jukwaa la kawaida.
No comments :
Post a Comment