Na Philemon Solomon wa Fullshangwe-Dar es salaam
BENKI ya Commercial of Africa Tanzania Limited imeanzisha promosheni ambapo wateja wake watanufaika na zawadi mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki hiyo, William Mungai
alisema promosheni hiyo itasaidia kuboresha maisha ya wateja wao na
wafanyakazi wa benki hiyo.
Alisema promosheni hiyo kwa mwezi itahusisha makampuni, wateja
binafsi ambapo mteja atatakiwa kufungua akaunti mpya kwa kiwango cha
chini cha milioni 50 ataingia kwenye droo ya kujishindia Laptop.
Alisema mteja akiweka pesa marambili zaidi kwenye akaunti yake ya
Current kwa kiasi kisichopungua milioni 20 naye ataingia kujishindia
Laptop.
"Mteja atakaye mshawishi mshirika wake mfanyabiashara, SME,
Msambaji, rafiki kufungua akaunti kwa kiasi kisichopungua milioni 15
ataingia kwenye droo ya kujishindia kompyuta ya mezani''. alisema
Mungai.
Aliongeza kuwa watu wote watakaokidhi vigezo cha kwanza na cha tatu wataingia kwenye droo kubwa ya kushinda kompyuta na printa.
Alisema kwa wateja binafsi wanapaswa kufungua akaunti mpya kwa
kiwango cha chini cha milioni 1 na kuiongia kwenye droo ya kujishindia
Tv ya Plasma.
Alisema mteja akiweka fedha zaidi ya mara mbili katika akaunti yake
kwa kiasi kisichopungua sh. milioni 500 ataingia kwenye droo ya
kujishindia DVD Home Theater.
Alisema kwa mtu atakaye mshawishi rafiki, mshirika na kufungua
akaunti ya familia yaani mke na mtoto mmoja kwa kiasi kisichopungua sh.
milioni 1 ataingia kwenye droo ya kujishindia TV ya Plasma.
Alisema kwa wateja watakaoingia robo mwaka ambapo itakuwa ni mwisho
wa kampeni na kukithi vigezo namba moja na tatu wataingia kwenye droo
kubwa ya kushinda Friji, DVD Home Theater na TV Plasma.
No comments :
Post a Comment