Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, June 3, 2012

Daryl Peoples Rais wa IBF/USBAA atunukiwa cheti


Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi kulia akimkabidhi cheti cha kutukuka Rais wa Shirikisho hilo duniani Daryl Peoples wa Marekani katika sherehe iliyofanyika kwenye Hotel ya Hawaiian Hilton Village Resort, jijini Hawaii, nchini Marekani.


Kampuni ya Kitwe General Trading ya jijini Dar-Es-Salaam inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bwana Lucas Rutainurwa imelitunuku cheti cha heshima Shirilisko la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA). Sherehe za kukabidhi chezi hicho zilifanyika katika jiji la Honolulu, Hawaii nchini Marekani na Kitwe iliwakilishwa na Rais wa Shirikisho la IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitwe General Trading, Rais Ngowi alisema kwamba IBF/USBA imetunukiwa kwa juhudi zake za kuendeleza mchezo wa ngumi katika bara la Afrika ambazo zinachangia sana katika kukuza ajira na biashara ya Utalii.
 
Naye Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani alimshukuru sana bwana Rutainurwa kwa juhudi zake za kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania. Peoples aliahidi kwamba atamsaidia Bwana Rutainurwa ili kuifanya Tanzania iwe ni Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika.

No comments :

Post a Comment