Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, June 8, 2012

KHADIJA KOPA KUIPAMBA MISS LAKE ZONE INTERCOLLEGES 2012



 
   Malkia wa mipasho na mshindi wa tuzo za Tanzania Kili music Awards 2012 Khadija Kopa anategemewa kuwa kivuto kikubwa kwa kutoa burudani ya kipekee katika shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS lAKE ZONE INTERCOLLEGES 2012 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Kagera katika mji wa Bukoba.
  Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es salaam Mwandaaji wa shindano hilo Bw.Joseph Rwebangira amesema kuwa asilimia kubwa ya maandalizi yameshatimia,hata hivyo Rwebangira aliongezea kuwa mshereheshaji wa siku hiyo atakuwa mchekeshaji maarufu afrika mashariki na kati Mpoki wa the origina comedy.
   Miss Lake zone Intercolleges 2012 inayoandaliwa na kampuni ya Angles Real Entertainment ya jijini Dar es salaam chini ya Mkurugezi wake Joseph Rwebangira imejipanga vya kutosha kuleta mabadiliko ikiwa na lengo la kumfikisha mrembo wake katika ngazi ya fainali kitaifa.
   Shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Linuz Club uliopo Bukoba mjini siku ya jumamosi tarehe  23 juni ambapo mbali ya hayo kutakuwa na burudani za ngoma za asili na wasanii wa mkoa wa Kagera,pia kiingilio kitakuwa ni Tsh 10,000/= kawaida na V.I.P ni Tshs 15,000/=

No comments :

Post a Comment