Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, June 10, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA KWANZA YA TANZANIA HOMES EXPRO



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa, NHC, kutoka kwa Ofisa Masoko wa Shirika hilo, Mariam Ndabagenda, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo, William Genya (wa pili kulia) ni Ofisa Mauzo mwandamizi wa Shirika hilo, Emmanuel Lymo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utengenezaji wa Viage vya ujenzi wa Nyumba kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kampuni ya Insignia Ltd, Obed Machoka, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba 220 zinazojengwa eneo la Jangwani Beach, jijini Dar es Salaam, zinazotarajia kutumia jumla ya Sh. Milioni 208, kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Global Land Solutions Ltd, Murtaza Adamjee, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu matumizi ya Nyaya za Africab kutoka kwa Ofisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Khuzema Janowalla, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments :

Post a Comment