Meneja
Mawasiliano wa kampuni ya ya Serengeti, Imani Lwinga, akizungumza na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge jijini Dar es
salaam leo, wakati kampuni hiyo ilipotangaza zawadi kwa washindi wa
tuzo za mwanamichezo bora wa TASWA, (kulia) ni Katibu mkuu wa
TASWA Amir Mhando na (katikati) ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
******************************
CHAMA
cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) kikishirikiana na
Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) leo wametangaza rasmi zawadi za
washindi wa Tuzo hizo na vipengele vya vigezo vitakavyotumika katika
kutoa tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka 2012, zoezi litakalodhaminiwa
na kampuni hiyo ya SBL.
Tukio
hilo la kuwatambua na kuwatunukia Tuzo wanamichezo bora wa 2012, ambao
wamejikita katika michezo na kuleta mabadiliko mbalimbali katika tasnia
ya michezo litafanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es
Salaam Juni 14, na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 1000.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jana, Meneja wa mawasiliano wa
kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Imani Lwinga amesema maandalizi juu ya
tukio hilo yanaendelea vizuri, ambapo kwa niaba ya SBL Meneja huyo
ameishukuru timu nzima ya TASWA kwa ushirikiano wa mzuri na kuigwa.
“Tunatambua
umuhimu na uwepo wa kila mmoja wenu katika maandalizi haya na
tunajivunia kuwa sehemu muhimu katika maandalizi ya tukio hili muhimu”
alisema Lwinga.
Aliongeza kuwa vipengele vilivyoanishwa katika tuzo hizo ni sahihi na kwamba kila kipengele kimewasilishwa kwa umakini mkubwa
mojawapo
wa kuwatambua waandishi wa habari za michezo, lakini pia kupitia
udhamini huu, tungepe kuwashauri waandishi hawa wa michezo kujaribu
kuangalia mbele zaidi ili kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii
juu ya tasnia hii na faida zake kwa jamii hasa hapa kwetu
Tanzania”alisema Lwinga.
Vipengele
vilivyoanishwa katika tuzo hizi ni kama ifuatavyo ambapoa
vilevipengele vyenye mshiriki zaidi ya mmoja ni zitahusisha
zitazingatia jinsia, Mshiriki wa tuzo za dhahabu watakuwa watatu,
Mchezaji wa kiwango cha juu,( wa kulipwa) na mchezaji wa kawaida nafasi
mbili.
Mshindi
wa jumla katika tuzo hizo atazawadiwa dola za kimarekani 8,000
zitakaoztolewa na wadhamini wakuu wa tuzo hizo Kampuni ya bia ya
Serengeti
No comments :
Post a Comment