SHIRIKISHO
la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa
Tanzania (TPBC) vyatuma salamu za rambirambi na kumlilia bingwa wa IBF
wa mabara na bingwa wa dunia wa WBU Magoma Shaban.
Magoma
aliyefariki jana katika hospitali ya Bombo jijini Tanga atakumbukwa kwa
umahiri wake katika mchezo huo wa ngumi za kulipwa.
Safari
ya Magoma Shaban kwenye ngumi za kulipwa ilianzia katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga mwaka 1998 wakati Onesmo Ngowi akiwa ndio kwanza
ameteuliwa na Rais wa zamani wa IBF Robert Lee Sr, kutoka nchini
Marekani kuanzisha shirikisho hilo la IBF katika bara la Afrika.
Katika
pambano hilo lililofanyika uwanja huo wa Mkwakwani, Magoma Shaban,
alipigana na Joseph Waweru kutoka Kenya na kumshinda kwa KO na
kutangazwa kuwa bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa Flyweight.
Mwaka
2000 Magoma chini ya kamouni ya Capital Promoters Limited chuini ya
mwandishi wa bahari mahiri bwana Gabriel Nderumaki alipigana na bondia
Totim Lukunim toka Thailand katika ukumbi wa PTA kugombea mkanda wa IBF
wa mabara katika uzito wa Flyweight na kumshinda kwa KO katika raundi
ya 4. Huo ndio ukawa mwanzo wa magoma Shaban kwenye kwenye matawi ya juu
katika ngumi.
Magoma Shaban alipigania ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italy na kumshinda bondia Ferid Ben Jeddou kwa TKO katika raundi ya 6.
Magoma alikuwa ni bondia aliyeing'arisha Tanzania na bara zima la Afrika katika medani ya ngumi za kulipwa duniani.
Kwa
mantiki hiyo leo IBF imetangaza rasmi kuuita mkanda wa uzito wa Fly
aliokuwa anachezea Magoma kuwa "Mkanda wa Magoma Shaban" katika
mapambano yote yatakayokuwa yanachezezwa katika uzito huu yatajulikana
kama "Ubingwa wa IBF Africa wa Magoma Shaban".
Tunafanya
hivi ili kuwaenzi mabondia wanaoleta mchango mkubwa katika medani ya
ngumi na hivyo majina yao kubakia katika kumbukumbu zetu milele.
Mola alitoa na Mola ametwa, jina lake lihidimiwe milele. Amin!
No comments :
Post a Comment