Baadhi ya Maofisa wa benki ya CRDB
Ofisa
Uhusiano wa benki ya CRDB, Nasib Kalamba akifafanua jambo kwa wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Azania, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na
benki hiyo, wakati wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha,
yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Habari Mseto Blog
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB wakiwa katika bandfa la benki hiyo.
Wateja wakipata huduma
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza katika viwanja hivyoAfisa Mikopo wa Wajasurimali
wadogo naWakati Frank Peter alisema kuwa
wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto za mitaji na kukosa elimu sahihi juu
ya kuweza kukopa katika taasisi za fedha.
Alisema kuwa na wajasiriamali wanatakiwa kupata elimu juu ya
kuweza kukopa ambapo CRDB inafanya hivyo kutoa elimu mbalimbali juu ya huduma
ya mikopo.
Alisema kuwa mikopo katika benki hiyo ni kuanzia sh.milioni
1 hadi 500 ambapo dhamana anatakiwa kuwa na mtaji wake kuanzia milioni 3 na
kuendelea pamoja na biashara yake kuwa imesajiliwa kupitia mamlaka husika
ikiwemo kuwa na utambulisho wa TIN.
Peter alisema katika kutoa mikopo wanaangalia pamoja na mzunguko wa biashara ya mteja ili
kujiridhisha juu ya kuweza kupata mkopo ikiwemo na dhamana ya mali zisizo
hamishika na mali nyingi wateja kuwa na nyumba kama sehemu ya dhamna ya mkopo.
Alisema kigezo kingine ni kuangalia umri wa biashara ambao kwa CRDB ni kuanzia miezi sita na kuendelea
No comments :
Post a Comment