Wagombea
Urais wa Marekani Mitt Romney (kushoto) na
Barack Obama wakishambuliana kwenye mdahalo uliofanyika alfajiri ya
kuamkia leo majira ya saa 10:00, kwa saa za Afrika Mashariki. Pamoja na
wadadisi wa masuala ya kisiasa hawakuridhishwa na kitendo chao cha kuto
jibu maswali
moja kwamoja badala yake walikua wakishambuliana.
Mdahalo huo wa pili
uliofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Hofstra huko Long Island unaonekana kumrejesha kwenye chat Rais Barack Obama, kwa kishindo dhidi ya mpinzani wake wa
chama cha Republican Mitt Romney kwa kumfunika
Mdahalo huo wa pili kati ya midahalo mitatu iliyopangwa kufanyika
umewapa nguvu wanachama wa Democrats waliokuwa wana hofu baada ya Obama
kufanya vibaya kwenye mdahalo wa kwanza wiki mbili zilizopita.
Obama ametetea sera zake na kumchallenge Romney kwa kubadilisha
badilisha misimamo kwenye masuala muhimu na kudai kuwa sera za mpinzani
wake zitawapendelea matajiri kama akichaguliwa.
Kwa mujibu wa kura za CNN, Obama amefanya vizuri kwa asilimia 46
dhidi ya Romney aliyepata asilimia 39.
Zaidi ya tweets milioni 7 zimeandikwa wakati wa mdahalo huo. |
No comments :
Post a Comment