Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli
(waliokaa mbele wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, kuhusu utaratibu wa usajili wa magari ya Umma
na kuwepo kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali
imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na
namba za kiraia yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .
Baada
ya hapo Operesheni kamata kamata magari, pikipiki, Bajaj na mitambo ya
umma, itaanza na vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili
zitakazotumika kama ST, PT, MT, JW, DFP, CW, SM na SU.
Kwa mujibu
wa Dk. Magufuli, hadi sasa serikali imeshasajili vyombo vya moto,
123,431 yakiwemo magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma. Mkuu wa
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga.
PICHA/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO
|
No comments :
Post a Comment