Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, October 27, 2012

HABIBU KINYOGOLI AENDELEA KUMKUMBUKA MWALIMU NYERERE KATIKA MICHEZO



MWALIMU Julius Kambarage Nyerere kipindi yuko madarakani, alipenda michezo kuanzia mashuleni hadi kwenye makampuni na mashirika mbalimbali hapa nchini, ingawa alikuwa akipenda mchezo wa bao.
Aliweka sera bora ya michezo na kufanikisha kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1967 na kutoa fursa zaidi kwa wenye vipaji kuvionyesha.
Kwa mujibu wa bondia mahiri wa Ngumi hapa nchini, Habibu Ally Kinyogoli (64), Nyerere alifanikisha wachezaji wa Tanzania kuitangaza zaidi nchi yetu na kufanya vizuri kutokana na mazingira bora yaliyokuwako wakati huo.
Kinyogoli ni mwanachama wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, Simba lakini hahudhurii michezo ya timu hiyo, mapenzi yake yanabaki kwenye ngumi.
Nyota yake ya michezo ilianzia shuleni, Manerumango Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mwaka 1958, alicheza soka, ngumi na riadha, aliendelea na mchezo wa ngumi kwa sababu ndio ulikuwa ndani ya damu yake, michezo mingine ilimshinda kwa sababu ya hasira za baadhi ya wachezaji pindi zinapotokea rafu.
Kinyongoli wakati alipokuwa akicheza, alikuwa pia akitoa mafunzo kwa wenzake, mwaka 1966, katika klabu ya Magomeni Centre yalipo makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni alimfunza Majuto Mahavu ambaye baadae alikuwa tishio kwenye timu ya Taifa.
Mwaka 1970 alijitosa rasmi kwenye ngumi baada ya kuvutiwa na Titus Simba aliyeiletea medali ya kwanza Tanzania ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Scotland, ndipo na yeye akaongeza ufanisi zaidi katika mchezo huo.
Mwaka 1971 aliajiriwa kiwanda cha Bora baada ya kuonesha umahiri katika mchezo huo, akafanikiwa kumfudinsha ngumi, Zakaria Yombayomba, mwaka 1973 aliasisi klabu ya ngumi ya Urafiki akawaibua akina Charles Mhilu ‘Spinks’, Habibu Mzungu, Lazaro Makarious, Kwelu Msinjili na wengineo.
Mwaka 1972 alishiriki mashindano ya Olimpiki, Munich Ujerumani walikwenda na akina Titus Simba, Robert Mwakosye, Bakari Suleimani ‘Match Maker’, Said Tambwe katika mashindano hayo, mwanariadha Clever Kamanga aliipa Tanzania medali ya shaba kwa mbio za umbali za mita 400.
Katika mashindano hayo, Kinyogoli alifanya vibaya baada ya kukatika kwa mshipa wa mkono wa kulia katika mazoezi nchini humo, mchezo wa kwanza wa Olimpiki alishinda kwa pointi nyingi dhidi ya Mcambodia, mchezo wa pili alipoteza pambano baada ya kujitonesha mkono wake na damu zikatoka nyingi.
Maumivu hayo hakuyaona hadi, Profesa Philemon Sarungi wakati huo alikuwa akisoma nchini humo, alijitolea kuisaidia timu hiyo.
Mwaka 1973 alishiriki All Africa Games jijini Lagos Nigeria akarejea na medali ya fedha na kuchaguliwa kwenye timu ya Afrika iliyoshiriki Inter-Continental  iliyofanyika Mexico , uteuzi huo pia uliwahusu pia akina Jacob Mussa, Bakari Suleimani, Titus Simba na Mbaraka Mkanga wakati katika soka Tanzania iliwakilishwa na akina Maulid Dilunga, Abdallah Kibadeni na Kitwana Manara.
Mwaka 1974 alisisi klabu ya Simba ambayo kipindi hicho ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Abubakar Mwilima baada ya kuchana mkataba wa Bora, baada ya uongozi mpya wa kiwanda hicho kutokupenda michezo, akaondoka na wenzake wote aliokuwa nao kiwandani hapo kama Bakari Suleiman ‘Match Maker’, YombaYomba na wengineo.


1976 akiwa kwenye kambi ya maandalizi ya Olimpiki alitangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa, mwaka 1978 akaanzisha klabu za watoto wadogo ya Relwe na kuendelea na Simba, Simba wakachipukia akina Rashid Matumla, Iraq Hudu Mkumwena,Rajabu Mhamila 'Super D' Shabani Mhamila 'Star Boy, Remmy Ngabo, Joseph Marwa,mohamedi Chipota na wengineo.
Hivi sasa, Kinyogoli anafundisha klabu ya Amana ya Ilala akisaidiwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' kocha Mohamedi Chipota, Kondo Nassoro na Sako Mtulya na akiendelea na Simba pia akiwa na changamoto nyingi ambazo ni uwezeshwaji wake kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sababu ameutengeneza mchezo huo tangu alipokuwa akifanya kazi na alitumia gharama zake lakini sasa, kazi hafanyi. Ametoa wito kwa mashirika na watu binafsi waliokuwa na nia ya kumsaidia
kuendeleza mchezo wa masumbwi nchini kuja katika kambi ya Ilala Iliyopo
Amana CCM ambapo ana endesha darasa la vijana kujifunza na kujiendeleza kwa
mchezo uho au anaweza kuwasiliana moja kwa moja na habibu Kinyogoli kwa
simu namba 0655928298

No comments :

Post a Comment