USHINDI
kutoka kwa Toto African ya Mwanza katika mechi ya juzi kwenye Uwanja wa CCM-
Kirumba, umewapa usongo mabingwa hao mara 24 wa Bara tangu mwaka 1965, ambapo
sasa wameapa hakuna kulala katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu.
Ikitoka
kulimwa bao 1-0 na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, juzi ilizinduka na
kushinda mabao 3-1, hivyo kufikisha pointi 11, ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya
kinara Simba na Azam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam
jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako alisema kikosi cha timu hiyo
kilitarajiwa kuwasili jana usiku, kuendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na
mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting itakayocheza Oktoba 20.
Mwalusako,
beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ernie
Brandts, ataanza rasmi progamu yake kwani kikosi chake kitakuwa kamili, hivyo
kubaini dosari zilizojitokeza kwenye mechi kadhaa zilizopita.
“Unajua
tangu kocha aanze kazi, hajapata muda wa kutosha kuwajua vizuri wachezaji,
hivyo kwa siku za kujiandaa na mechi ya Ruvu Shooting, ataangalia maeneo gani
yatapaswa kufanyiwa kazi ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo,”
alisema.
Mwalusako
aliongeza kuwa, ushindi kutoka kwa Toto ni faraja, na kitu muhimu kwao ni
kuongeza juhudi zaidi kushinda mechi zijazo kuzidi kujiongezea pointi.
Katika hatua
nyingine, Mwalusakao alisema wameandika barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kuomba mechi yao
kuhamishwa kutoka Azam Complex hadi Uwanja wa Taifa kwa hoja ya kutoa nafasi
kwa wapenzi na mashabiki wengi kushuhudia.
No comments :
Post a Comment