Mashambulizi ya mapema ya David Price (kushoto) kwa Audley Harrison
yalianza hivi Ukumbi wa Lecho Arena jijini Liverpool, England jana.
Kisha mashambulizi hayo ya David Price (kulia) yakamlazimisha Audley
Harrison (kushoto) kujisalimisha kambani na kuzuia hatari zaidi.
Ndipo makombora mazito mfululizo ya Price, yalimpomzidi uwezo Harrison
na kuanguka ulingoni, ambapo hapa mwamuzi anajaribu kumdaka bila
mafanikio. Hii ilikuwa ni dakika ya kwanza sekunde ya 22.
LIVERPOOL, England
Kwa muda mfupi wa pambano hilo, Harrison alikuwa na kazi
moja ya kukwepa makonde mfululizo aliyokuwa akimiminiwa na Price, ingawa mawili
mazito yalimpata vema – kabla ya kuanguka na kukimbizwa hospitali akiwa anapumulia
mashine
BONDIA Audley Harrison jana Jumamosi amenusurika kifo ulingoni, baada ya
kupigwa vibaya katika sekunde ya 82 tangu kuanza kwa pambano lake dhidi ya
mpinzani wake David Price aliyekuwa akitetea vema ubingwa wa Uingereza.
Harrison alilazimika kukimbizwa hospitali huku akipumulia
mashine, baada ya kukumbana na makombora mazito kwenye Ukumbi wa Echo Arena jijini Liverpool, kuwania ubingwa wa Uingereza
na Jumuiaya ya Madola uzani wa ‘heavyweight.’
Bingwa huyo wa zamani wa Olimpiki, alivunjika pua na kuvuja
damu kwa wingi, kabla ya kukimbizwa hospitali kuokoa maisha yake baada ya
kufeli kwa huduma za kwanza ulingoni hapo.
Kwa muda mfupi wa pambano hilo, Harrison alikuwa na kazi
moja ya kukwepa makonde mfululizo aliyokuwa akimiminiwa na Price, ingawa mawili
mazito yalimpata vema – kabla ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.
Akizungumzia ushindi wake, Price, 29, aalidai: “Umalizaji
wangu pambano ulikuwa mzuri kama nilivyoonesha. Lazima nikiri pia kuwa mimi
mwenyewe ilitisha wakati mwingine. Mara baada ya mimi kusikia harufu ya damu,
nikajua nimemaliza kazi.
“Nina heshima kubwa sana kwa Audley kutokana na alichowahi
kufanya ulingoni. Acha tupate kujua ukweli juu ya hali yake, yeye ni bingwa wa
zamani wa Ulaya – ambaye aliwania ubingwa wa dunia dhidi ya David Haye na mimi
niko mbali naye.
“Ukweli ni kuwa nina furaha. Najivunia kuwa Mwingereza. Nataka
kuhakikisha nchi hii inajivunia pia uwapo wangu kama bondia.”
Ushindi huo wa Price ulikuwa wa 14 katika mapmbano yake,
ukiwa ni KO ya 12 na pia ni pambano lake la sita kumshinda mpinzani katika
raundi ya kwanza.
No comments :
Post a Comment