Meneja Mkuu wa Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Kilala Sendama akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Posta Duniani.
Meneja Mkuu wa Biashara wa
Shirika la Posta Tanzania, Kilala Sendama akimkabidhi mmoja wa washindi
wa shindano la Uandishi wa Barua, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Kifungilo, Alvinar Alexander Mgoye wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani
iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Washindi wa shindano la Uandishi wa Barua wakiwa katika picha ya pamoja
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Posta Tanzania limefanikiwa kupata tuzo maalumu ya kimataifa kutoka
kwa Umoja wa Posta Duniani (UPU).
Mbali na hilo, shirika hilo limeanzisha vituo 36 vya kutoa huduma ya Internet katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha mfumo wa mawasiliano.
Mbali na hilo, shirika hilo limeanzisha vituo 36 vya kutoa huduma ya Internet katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha mfumo wa mawasiliano.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya siku ya
Posta duniani, Meneja Mkuu wa Biashara Tanzania Kilala Sendama alifafanua kuwa,
cheti hicho kimekuja baada ya shirika kupata alama ya 1,765 kati ya alama 2000
zilizokuwa zikishindaniwa.
“Cheti
hicho kinadhibitisha ubora wa huduma zinazotolewa na kilikabidhiwa kwa
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa mashirika ya posta, Yamungu Kayandabila,
vile vile tuzo hiyo itatumika kama kichocheo cha kuongeza ufanisi wa mafanikio
zaidi” alisema Sendama.
Katika
hilo alichanganua kuwa licha ya shirika kukabiliwa na changamoto lukuki katika
utoaji huduma endelevu, lakini limekuwa miongozi mwa historia ya mabadiliko
chanya hususani katika mtandao wa dunia kuanzia ngazi ya Kitaifa pamoja na
Kimataifa.
Sendama
alitabanaisha kwamba mbali na tuzo hiyo, shirika limetoa tuzo kwa Wanafunzi 10
katika shule za Sekondari nchini walioshinda vizuri katika shindano la Uandishi
wa Barua kwa ngazi ya kitaifa kwa mwaka 2012.
Aidha,
aliwataja washindi hao ni Alvinar Mgoye kutoka shule ya sekondari Kifungilo,
Mary Kilapilo sekondari ya Usambara,Sonia Chiliko Kifungilo, wote wa Mkoani
Tanga, Nyinga Jackson kutoka sekondari ya Ilboru Mkoani Arusha, pamoja na Anway
Omary kutoka shule ya Azania Dar es Salaam.
Aliwataja
wengine ni Violet Richard kutoka shule ya sekondari St Joseph Mkoani Mwanza,
Edith Mkwawa, Sylcheria Kaole, wote kutoka Usambara Korogwe, Raya Mwamwetta
kutoka Kifungilo Mkoani Tanga, pamoja na Faraj Azizi kutoka shule ya sekondari
Ummu Salama Mkoani Iringa.
Akizungumza
kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliopewa tuzo hizo, Mary Kilapilo alitumia
fursa hiyo kuwataka wanafunzi wengine kuipenda huduma hiyo kwa sababu
inawapunguzia matatizo mbalimbali likiwemo la kutojiingiza katika vishawishi
vya mapenzi.
No comments :
Post a Comment