Onesmo Ngowi |
OKTOBA 22, 2012
Gazeti la Mwananchi ni moja ya magazeti
yenye wasomaji wengi sana hapa Afrika ya Mashariki kutokana na uandishi
wake uliobobea kwenye utafiti. Mara nyingi gazeti hili limekuwa linaibua
ukweli kwenye masuala mengi yanayohusu jamii. Hili linalipa heshima
pekee kama gazeti la watu na sio tu hapa Tanzania bali ni Afrika hata
dunia nzima.
Kazi kubwa ya uandishi ni kuandika ukweli
na ni muhimu kwanza ukafanyika utafiti ili ukweli wenyewe usije
ukawaumiza wake ambao unataka kuwasaidia. Ni muhimu habari yenyewe
inayoandikwa iwatendee haki wale wote unaowagusia.
Pamoja na heshima hii ya gazeti la
Mwananchi tuna shaka na uandishi wa mwandishi mmoja anayeitwa Imani
Makongoro ambaye anajaribu sana kujihesabu kama mwandishi mtaalam wa
wasuala ya ngumi. Mwandishi huyu amekuwa anaandika habari ambazo hazina
ukweli na hazikufanyiwa utafiti.
Aidha amekuwa anakurupuka kuandika habari
ambazo haziwatendei haki wale anaowaandika kwa maana ya kuwahoji kwanza
kabla ya kuandika kama yalivyo maadili kwa mwandishi yeyote aliyesomea
kazi ya uandishi wa habari.
Pamoja na habari zake nyingi ambazo hazima
kichwa wala miguu kuhusu tasnia ya ngumi, leo hii amekuja na habari
(piece) inayosema “TPBO, PST na TPBC achene kuwadanganya mabondia wa
Tanzania”.
Mwandishi huyu amedai kuwa TPBO, PST na
TPBC vimekuwa vinawatengenezea mabondia wa Tanzania mikanda isiyo na
maana ya heshima stahiki. Ameendelea kuorodhesha umbumbumbu wake kwa
makala ndefu isiyo na kichwa wala miguu kuhusu mchezo wa ngumi za
kulipwa. Hii ni hatari kubwa sana kwa mwandishi anayeliandikia gazeti
linalioheshimiwa kama Mwananchi kuandika habari asizosijua.
Makongoro amekuwa na tabia ya kupekua sana
kwenye internet na kudurufu habari zilizoandikwa na wengine huko kwa
mtindo wa “copy and paste” au “bandua bandika” na huu umekuwa ndio
mtindo wake wa uandishi wa habari siku zote! Ukisoma kwa uangalifu
makala zake ni zile ambazo hazijafanyiwa utafiki ila ni za umbea wa juu
juu tu!
Imani Makongoro kweli kafulia kwa maana
hata hajui duniani kuna mashirikisho mangapi ya ngumi za kulipwa. Hajui
hata sababu ni kwa nini mashirikisho, mabaraza au vyama vingapi vya
ngumi za kulipwa vilianzishwa duniani.
Katika makala zangu za “Mchezo wa Ngumi,
Taa inayozizima” na ambazo zinaendelea (niko kwenye sehemu ya kumi na
nane) nimekuwa naeleza kwanini duniani kuna mabaraza, vyama au
mashirikisho mengi ya ngumi za kulipwa na faida zake ni nini!
Pengine Imani Makongoro huwa hasomi makala
hizi zilizoandikwa na mimi kama mtaalam wa masumbwi nisiye mumunya
maneno. Nasema mimi ni mtaalam kwa kuwa nimecheza ngumi za ridhaa,
kulipwa na sasa naongoza taasisi zinazoheshimiwa duniani ambazo Imani
Makongoro mwenyewe hazijui.
Kwa ufupi mimi ni Rais wa Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Rais wa Chama Cha Ngumi Za KUlipwa
Afrika ya mashariki na Kati (ECAPBA), Mkurugenzi wa Baraza La Ngumi la
Jumuiya ya Madola (CBC) na Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na
Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) katika bara la Afrika, Mashariki
ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi.
Hizi sio taasisi ndogo na mimi nimekuwa
"Mtu wa Kwanza kutoka bara la Afrika" kuweza kufikia katika nafasi
niliyo nayo kwa sasa na inaipa nchi yangu Tanzania heshima kubwa sana
duniani.
Ndiyo maana mabondia kama kika Francis
Cheka, Rajabu Maoja, Magoma Shaaban (Marehemu), Rogers Mtagwa, Bakari
Mambea, Thomas Mashali, Ramadhani Shauri, Manda Maugo, Mbwana matumla,
Rashid Matumla, Joseph Marwa, Maneno Oswald, na wengine wengi wameweza
kupata nafasi za kupigania matuzo mbalimbali ya mashirikisho haya!
Lakini kwenye kumbukumbu za Imani Makongoro yete ngumi Tanzania anamjua tu Rashid Matumla wengine kwake hawana maana yoyote!
Inanipa taabu kubwa kujaribu kufikiria ni
sababu gani haswa iliyomfanya Imani Makongoro kuandika habari (piece)
inayowadhalilisha viongozi wa TPBO, PST, TPBC na wadau wote wa ngumi za
kulipwa Tanzania.
Kinachoweza kuelezwa ni labda ametumwa na
baadhi ya watu ambao wamekuwa wanamtumia kuchafua TPBO, PST na TPBC.
Mabwana au mabibi hawa waliomtuma Imani Makongoro wanasahau jambo moja
kubwa kuwa “Ni Michezo wa Ngumi za Kulipwa pekee unaoitangaza Tanzania
vizuri katika medani ya michezo duniani” kwa sasa.
Imani Makongozro alinipigia simu jana na
kuniuliza ni kwanini simpatii Francis Cheka pesa za mazoezi na
nikamwambiwa kuwa sheria ya mikataba ya ngumi za kulipwa haziruhusu
kinachoitwa pesa za awali (Advance Payments)!!
Lakini kwa watu wa aina ya Imani Makongoro
hawaelewi lolote utakalowaambia. Anachojua ni kukimbilia na kuandika
habari zisizo na kichwa wala miguu!
Nilimwambia kuwa Francis Cheka hana meneja na kama anadai kuwa ana meneja basi amwonyeshe mkataba wake wa meneja!
Lakini kama nilivyokwisha sema hapo juu,
Imani Makongoro hawezi kusikia au kuona hili badala yake amejaa mahasa
za kukimbilia kuandika habari ambazo hazina kichwa wala miguu ili
kuwadhalilisha wadau wanaohesimika katika medani ya ngumi za kulipwa!
Sisi TPBO, PST na TPBC hatuna magazeti ya
kumwandika Imani Makongoro. Yeye na mhariri wake wa michezo wa gazeti la
Mwananchi wala kila sababu za kuringa kwa kuwa wanalo jukwaa (forum) ya
kutudhalilisha na kutuharibia heshima yetu kwa jamii.
Mahali pekee tunapoweza kukutana naye ili aweze kuthibitisha tuhuma alizozitoa kwetu ni “MAHAKAMANI PEKE YAKE!
Sisi TPBC tutakwenda mahakamani ili Imani
Makongoro athibitishe tuhuma zake kuhusu "udanganyifu tunaoufanya kwa
mabondia wa Kitanzania".
Imeandikwa na:
Onesmo Ngowi
Rais,
KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA (TPBC)
Chama Cha Ngumi za Kulipwa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)
Barala la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC)
IBF Africa, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi
No comments :
Post a Comment