Bondia kutoka nchini Namibia Gottlieb
Ndokosho ambaye alimsambaratisha Mtanzania Rajabu Maoja katika raundi ya
kwanza ya mpambano wao wa kugombea mkanda wa IBF Afrika katika uzito wa
unyoya, atapanda tena ulingoni jijini Windhoek, Namibia kutetea mkanda
wake kati ya mabondia watatu ambao walipendekezwa na IBF.
Pambano
hilo litakalofanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia utatoa
upinzani mkali sana kati ya mabondia hao wanaochipukia vyema.
Kati ya majina matatu yaliyopendekezwa na
IBF limo jina moja na Mtanzania Fredy Sayuni ambaye anaishi jijini
Dar-Es-Salaam. Wengine ni Patric Okine kutoka Ghana na David Kiilu
kutoka nchini Kenya.
Wakati huo huo IBF
imetoa kibali kwa bondia Helene Joseph wa Nigeria kutoka barani Afrika
kupigania ubingwa wake wa dunia. Mpambano huo utawakutanisha Helen
Joseph kutoka nchi ya Nigeria akikutana na bondia Dahianna Santana
kutoka Dominican Republic huko Latin America ambaye ndiye bingwa wa
dunia wa IBF katika uzito wa unyoya (featherweight) kwa upande wa
wanawake.
Helen Joseph
Mpambano
huo utafanyika Decemba 1 katika jiji la San Domingo na litasimamiwa na
Rais wa IBF kutoka bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na
Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi.
Picha ya (kulia) Bondia Santana kulia, akiwa ulingoni.
Bondia
Helen Joseph ameshapigana mapambano 13 na amepoteza moja wakati
mpinzani wake Dahianna Santana amepigana mara 37 na kupoteza mara 6.
*Uongozi*
*IBF Africa, Masharikim ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi*
*Dar-Es-Salaam*
You might also like:
No comments :
Post a Comment