DANIEL AKUFF (KATIKATI) AKIWA AMENYANYUA DALUGA WAKATI AKIWANIA MPIRA
DHIDI YA AMRI KIHEMBA KULIA HUKU HARUNA SHAMTE AKIUPIGIA MAHESABU MPIRA
HUO.
UHURU SELEMAN (16) AKITAFUTA NAMNA YA KUWATOKA WACHEZAJI WENZAKE MWINYI KAZIMOTO.
WACHEZAJI WAKIOMBA DUA MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MAZOEZI.
MASHABIKI WA KLABU YA SIMBA WAKINGALIA MAZOEZI YA KLABU HIYO.
MENEJA wa klabu ya Polisi Moro Sport
Club na Msemaji wa klabu hiyo, Clement Bazo amesema kuwa klabu yake
itaibuka na ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara
klabu ya Simba katika mchezo wao wa ligi hiyo utaopigwa kesho kwenye
uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:30 mkoani hapa.
Bazo alisema kuwa mchezo huo utakuwa
mchezo wao wa tisa tangu kuanza kwa ligi hiyo na kupoteza michezo sana
na kutoa sare mbili na kujikusanyia pointi mbili wanauchukua mchezo huo
kama michezo mingine baada ya kufanya vibaya hivyo lengo kuu ni kufanya
vizuri na kuwa wamejindaa kukabiliana na vinara hao.
“Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa
michezo iliyobakia hivyo kesho (leo) tunacheza na Simba hivyo sisi
Polisi lengo letu tulilonalo kwa sasa ni kufanya vizuri ukiwemo mchezo
wetu dhidi ya dhidi ya Simba SC na tunaasilimia 75 ya ushindi kwa mchezo
huo”. Alisema Bazo.
Bazo alisema kuwa mchezo ni mchezo
matokeo ambayo yanahitajika katika mchezo huo kama watashindwa kuwafunga
Simba basi mchezo utaweza kumalizika kwa sare ya aina yo yote ile.
Naye Kocha Mkuu wa klabu ya Polisi Sport
Club, John Simkoko amesema maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Simba
yamekabili na anachosubiri ni dakika 90 kuweza kuamua matokeo ya mchezo
huo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya
simu kutoka jijini Dar es Salaam ambako wameweka kambi katika jeshi la
polisi Kulasini, Simkoko alisema kuwa wachezaji wake wote wapo fiti kwa
mchezo huo na anachosubiri ni kuanza kwa mchezo huo dhidi ya vinara wa
ligi ligi Simba Sport Club hii kesho.
Simkoko alisema kuwa waliweka kambi
mapema katika jiji hilo baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu JKT kwa lengo
kumalizia michezo iliyobakia ukiwemo na Simba katika uwanja wake wa
nyumbani na kuwa dakika 90 ndizo zitakazoamua mshindi katika mchezo wa
soka.
“Mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote
mbili na tumejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuikabili Simba hivyo
najua Simba wanahitaji ushindi nasi vile vile tunahitaji ushindi katika
mchezo huo lakini dakika 90 ndizo siku zote zinaamua matokeo ya mchezo
ikiwemo sare, kupoteza na ”. alisema Simkoko.
Katika mchezo huo utanarajia kuibua
hisia nyingine kutoka kwa mashabiki Manispaa ya Morogoro endapo klabu
hiyo ya Polisi Moro kama itaendelea kupoteza mchezo huo baada ya
kupoteza mwelekeo kufuatia kufungwa michezo saba na sare mbili huku
ikiwa na pointi mbili.
No comments :
Post a Comment