Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, October 19, 2012

SAFARI LAGER YAZINDUA MSIMU WA PILI WA PROGRAMU YAWAJASIRIAMALI YA “SAFARI LAGER WEZESHWA”.



 
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo(kulia) na Jaji ,Joseph Migunda kutoka kampuni ya TAPBDS wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa program ya Wezeshwa awamu ya pili iliyofanyika TBL Dar es SalaamMeneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa program ya Safari Wezeshwa awamu ya pili iliyofanyika katika Ukumbi wa TBL Dar es Salaam .Kushoto ni jaji wa program hiyo,Joseph Migunda kutoka kampuni ya

 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi msimu wa pili wa programu ya wajasiriamali ijulikanayo kama“Safari Lager Wezeshwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema kwamba programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya pili  inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya. Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwapa changamoto wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia ruzuku za programu ya“Safari Lager Wezeshwa” lakini kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu ya usajili na kutembelea website ya www.wezeshwa.co.tz.
Naye Bwana Joseph Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hiialisema kwamba sifa za kushiriki ni sawasawa na ilivyokuwa msimu uliopita. Alieleza kwamba wajasiriamali watakaojitokeza kushiriki wanapaswa kuwa na sifa kuu nne; wawe wachapakazi hodari, wawe wanamiliki biashara binafsi ambazo ni halali, wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na wawe na nia ya kukuza biashara zao ili ziweze kuwasaidia wao na jamii inayowazunguka. Bwana Migunda alieleza kwamba vigezo vinavyotumika kupata watakaofaulu ni pamoja na kufuata vizuri maelekezo ya ushiriki, kuwa na wazo ambalo ni la ubunifu zaidi, kuwa na biashara ambayo inasaidia jamii inayoizunguka biashara hii nk. Alimaliza kwa kusema kwamba “Natoa wito kwa wajasiriamali kote Tanzania wajiandae vizuri, watayarishe nakala sahihi za hati za biashara zao, wasome na kujaza vizuri kwa usahihi fomu za ushiriki mara zitakapotolewa na wawe na uhakika kabisa kwamba TAPBDS kama waratibu wa “Safari Lager Wezeshwa” tutahakikisha vigezo vilivyowekwa vinatumika vizuri katika kumpata mshindi wa kweli”. Kama ilivyokuwa mwaka jana, washindi msimu huu wa pili watawezeshwa kwa kupatiwa elimu ya biashara na ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana na biashara zao.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
  Mjasiliamali wa kutengeneza keki, Elizabeth Chami (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya bidhaa anazozalisha kutokana na mashine aliyowezeshwa awamu ya kwanza wakati wa uzinduzi wa program hiyo awamu ya pili iliyofanyika TBL Dar es Salam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mjasiliamali wa kutengeneza keki, Elizabeth Chami (kulia)akimuonyesha Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo baadhi ya bidhaa anazozalisha kutokana na mashine aliyowezeshwa awamu ya kwanza wakati wa uzinduzi wa program hiyo awamu ya pili iliyofanyika TBL Dar es Salam.

No comments :

Post a Comment