Katika mpambano uho bondia wa Kenya Matayo Keya alimtwanga kwa point bondia kutoka Tanzania Said Hofu na bondia Frank Mnene alimtwanga John Christian wa TZ nae Bondia wa Tz George Constantno alimtwanga Isack Meja
Na bondia wa kike kutoka Tanzania Sara Andrew alipigwa na bondia wa kike kutoka kenya Gronna Kusa katika atua nyingine bondia Denis Martin wa Tanzania alimtwanga Kamau Ng'ang'a wa kenya na bondia Mohamed Chibumbuli alimtwanga Edwin Okongo wa Kenya
Katika hatua nyingine Viongozi wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Masumbwi Nchini Kenya wamefurai kuwepo hapa kwa ajili ya kujipima nguvu kwa kuwa ni jumuiya moja ya Afrika Mashariki ambapo mashindano haya yalikuwa yakitokea mara kwa mara kipindi cha nyuma ambapo mabondia wengi walikuwa wanakwenda kenya na wengine kuja nchini kwa ajili ya kupima viwango vyao
Nawo viongozi wa Chama cha mchezo wa Ngumi za Ridhaa BFT Mwenyekiti Michael Changalawe amesema mabondia wa Kenya wamejigalamia wenyewe kutokana na kutokuwepo na wazamini ambapo wengi wao wameupa kisogo kuzamini mchezo wa Masumbwi nchini unaopendwa na mashabiki wengi hivyo amewataka wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia mchezo huu wa masumbwi
No comments :
Post a Comment