Willy akiwa Rais Jakaya Kikwete enzi za uhai wake |
MHARIRI wa Jamboleo, Willy Edward Ogunde amefariki dunia mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo (saa 6.30) usiku.
Taarifa
ya Neville Meena, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, imesema kwamba
Willy aliyewahi kuwa Mhariri wa gazeti la BINGWA, pamoja na wahariri
wengine walikuwa mjini Morogoro ambako walikwenda kuhudhuria mkutano wa
masuala ya sensa iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Mara
baada ya semina hiyo alikwenda kuwaona watoto wake na alikuwa huko hadi
saa sita usiku alipomwita dereva wa pikipiki afike kumchukua kwa lengo
la kurejea katika hoteli alikokuwa amefikia. Baada ya kutoka nje, na
hatua sita hivi kabla ya kufika pikipiki ilipokuwa, alianguka.
Ndugu
zake walimkimbiza hosipitali lakini walipofika na daktari kumpima,
tayari alikuwa “amenyamaza” yaani amefariki dunia. Taratibu za
kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es Salaam zinafanywa.
Tutamkumbuka
daima kwa upole na unyeyekevu wake. Kweli Willy ametuacha, ni pigo kwa
taaluma yetu, ni pogo katika Jukwaa la Wahariri. Poleni kwa familia ya
Willy Edward Ogunde, pole kwa wahariri wote na pole kwa tasnia nzima ya
habari. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
You might also like:
No comments :
Post a Comment