Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akimkabidhi katibu wa umoja wa wafanyabishara wa bodaboda msaada wa pikipiki 10.
Pikipiki 10 aina ya sanlag CC150 zilizotolewa msaada ya mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji kwa vikundi 10 vya wafanyabiashara wa bodaboda mjini Singida.
Baadhi ya wafanyabiashara wa bodaboda wa mjini Singida wakiserebuka na kucheza 'KIDUKU' na mbunge wao Mohammed Gullam Dewji muda mfupi kabla ya mbunge huyo kuwakabidhi wafanyabiashara hao msaada wa pikipiki.
Na Geofrey Mwakibete na Nathaniel Limu
Wafanyabiashara
wa bodaboda jimbo la Singida mjini,wamehimizwa kuunda/kuanzisha
vikundi ili pamoja na mambo mengine, kujijengea mazingira mazuri ya
kukopesheka.
Wito huo umetolewa na
mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,wakati
akizungumza kwenye hafla iliyofana, ya kukabidhi pikipiki 10 aina ya
sanlag CC 150 zenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa vikundi vya
wafanyabiashara wa bodaboda.
Alisema
faida za kujiunga kwenye vikundi ni nyingi ikiwemo ya kuwa nafasi nzuri
ya kupata mikopo mbalimbali kutoka kwenye taasisi za kifedha.Mtu mmoja
mmoja akitaka kukopa fedha benki ni ngumu, kuotokana masharti
yaliyowekwa na taasisi za kifedha.
“Siku
zote umoja ni nguvu,utegano unachangia kuleta ulegevu unaozaa
udhaifu.Mahali pana ulegevu,kwanza hakuna maendeleo ya kweli na pia
kutetea haki,inakuwa ngumu mno”,alifafanua Dewji ambaye pia ni mjumbe wa
NEC CCM mkoa wa Singida.
Kuhusu
pikipiki hizo alizotoa msaada, alisema lengo lake ni kwamba kila kikundi
kitaitumia pikipiki yake kwa ajili ya kukiongezea kikundi mapato ambayo
endapo yatatunzwa vizuri,ipo siku kila mwanakikundi anaweza akamiliki
pikipiki yake binafsi.
Aidha,
amewataka wakati wote kuzingatia sheria halali zilizowekwa na mamlaka
husika, ili shughuli zao ziweze kuendelea bila matatizo.
“Pia napenda kutumia fursa hii, kuomba mamlaka zinazohusika na sheria
za usalama barabarani na utozaji wa kodi na ushuru, kujipanga kwa ajili
ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa bodaboda,ili waweze kuzifahamu
sheria husika”,alisema na kuongeza;
“Nina
imani kwamba wafanyabiashara wa boda boda wakifahamu kwa kina sheria za
usalama barabarani,kutapunguza mno ajali na pia wakifahamu mambo ya
kodi na ushuru,hawatakwepa kulipa”.
Katika
hatua nyingine, Dewji amewahimiza waumini wa madhehebu ya dini,
kuongeza kasi ya utoaji sadaka,ili kuimarisha ustawi wa madhahebu yao.
Alisema
waumini wanao wajibu mkubwa wa kuchangia kwa hali na mali madhehebu yao
kwa lengo yaweze kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi zaidi.
“Sadaka
inayotolewa kwa moyo mkujufu,licha ya kusaidia ustawi wa dhehebu la
dini husika,mtoaji anakuwa amejiwekea thawabu mbele ya mwenyezi
Mungu”,alisema Dewji.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo,mbunge huyo, alisema ustawi wa kweli wa dhehebu la
dini,utaletwa na waumini wenyewe,watu wengine/taasisi zingine,kazi zao
ni kusaidia mahali waumini wanapokuwa wamepelea.
Katika
siku yake ya pili ya ziara yake ya kikazi jimboni kwake,Dewji alitoa
msaada wa mifuko ya saruji 40 kwa msikiti wa kijiji cha Manguamitogho na
mifuko mingine 25 ya saruji na shilingi laki tano taslimu, kwa kanisa
la Pentekoste la kijiji cha Ititi.
Katika
siku yake ya mwisho ya ziara yake (17/6/2012),Dewji alitarajiwa kuwa na
kikao maalum na madiwani wa kata za Singida mjini,kuzindua kisima cha
maji cha kijiji cha Mtisi,kuzungumza na wanachama wa klabu ya waandishi
wa habari mkoa wa Singida na kukagua kituo cha afya cha Sokoine mjini
Singida
No comments :
Post a Comment