Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Mwanasheria
Tike Mwampipile akizungumza na washiriki wa semina ya mapendekezo
ya
kuwepo kwa sheria ya Afya ya Uzazi Salama
katika mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya
iliyomalizika jana kwenye ukubi wa hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza
jijini Dar es salaam.
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
JAMII iimeshauriwa kulipa kipaumbele suala ya mapendekezo ya
kuwepo kwa sheria ya Afya ya Uzazi Salama
katika mchakato wa kuwepo kwa Katiba Mpya ,
ambayo itawezesha watumishi wa afya ambao watasababisha vifo vya
wakinamama
wajawazito au watoto wachanga kwa sababu
za uzembe.
Kauli hiyo
iliyoilitolewa (jana) na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Chama
cha Wanasheria Wanawake
Tanzania(TAWLA), Tike Mwampipile, wakati akifafanua
ya mapendekezo hayo
iliyoandaliwa na chama hicho kwa
waandishi wa habari kwenye semina ya siku mbili iliyofanyika , Ubungo
Plaza jijiini
Dares Salaam.Semina ya mafunzo hayo ambayo iliyoanza jana
(juzi) na kumalizika leo(jana)
“ Wito wangu katika jamii ni ni ina wajikubu mkubwa wa kujua
haki zao za msingi na kufahamu wapi pa kuzipata. Afya ya Uzazi Salama ni
kitu
muhimu ambacho hakijangaliwa kwa umakini. Hivyo katika mchakato wa
Katiba Mpya
suala hili liangaliwe kwa uzito kwa na
upana wake kujali mama ambaye analemta mtoto hapa duniani ambaye
anaweza kuwa na Rais au Waziri Mkuu wa kesho,” alisema Mwampipile.
Aliongeza kuwa kuwepo
kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza
idadi ya vifo vya wakinamama wajawazitio na watoto wachanga.
Kwa upande wake mtoa mada wa mapendekezo hayo, Bernadetha
Mkandya ambaye pia ni mjumbe wa
bodi ya TAWLA na Wakili wa Kujitegemea alisema kuwa
mwanamke ana haki ya kuishi na kulindwa ,hivyo sheria
hiyo
italuiwezesha taifa kupata watoto waliolelewa katika mazingira bora na
afya
njema. .
“ Tunataka tuwe na sheria ya iyatomlinda mwanamke wakati wa
ujauzito na siku 42 baada ya kujifungua,” ikiwepo kupanga
idadi ya watoto atakaoweza
kuwalea na muda wa kupata mtoto mmoja baada ya mwingine alisema.
Akifafanua zaidi
kuhusu sheria hiyo alisema itamwezesha
mamamjamzito kupata huduma za afya ya uzazi salama bora na ambazo
zitamwezesha
kupata vifaa tiba vinavyotakiwa bila gharama yeyote.
Aidha Mkandya aliongeza katika sheria hiyo wamapendekeza
kuwa umri wa uti mzima uwe ni miaka 18 ili kuwezesha mtoto wa kike
kuolewa
katika umri unaotakiwa hatua ambayo itasaidia kupunguza athari za afya
ya uzazi
zinazotokana na umri mdogo. Alisisitiza kuwa
ni muhimu kwa makundi yote katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya
mchakato huo.
Mkandya aliongeza kuwa mapendekezo hayo hayo yanaelekeza
kuwepo kwa sheria ambayo
itamwezesha mama mjamzito kusitisha ujauzito pale itakapogundulika kuwa
unasabbaisha athari za kiafya kwa ruhusa ya daktari na ridhaa yake
au endapo atakuwa amebakwa na kwa ridhaa yake kuwa
hana uwezo wa kuendelea
hudumia ujauzito huo na kumlea mtoto pale atakapojifungua.
No comments :
Post a Comment