Rais
wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani katikati akiwa amesimama na
Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
Onesmo Ngowi wa Tanzania pamoja na promota maarufu wa ngumi wa Thailand
Jimmy Chaichotchuang walipotembelea Pearl Habour tarehe 30 May, 2012.
Mkutano wa 29 wa Shirikisho la
Ngumi la Kimataifa (IBF) umeanza rasmi katika Hotel ya Hawaii Hilton
Village Resort jijini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 29 May, 2012.
Mkutano huu ulianza rasmi saa 3 za asubuhi katika ukumbi wa kimataifa wa
Atlatic International Conference Center, kwenye jengo la Rainbow Towers
katika hotel hii ya nyota tano.
Tarehe 29 ilianza kwa wajumbe wa
mkutano huo kujiandikisha kuanzia saa 3 za asubuhi mpaka saa 11 jioni.
Jioni wajumbe wote walikuwa na cocktail party ya get together katika
ukumbi wa Rainbow Towers.
Mkutano huu unahudhuriwa na
wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya
ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya
Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Akiwakaribisha wajumbe walioanza
kumiminika katika mkutano huo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa
Marekani aliwataka wakaribie Marekani na kutumia muda walionao katika
jiji la Honolulu kufahamiana na kutembelea jiji hili.
Ratiba ya siku tano itajumuisha
kuwa tarehe 29 ni siku ya kuanza kwa mkutano huo kwa wajumbe
kujiandikisha. Jioni kutakuwa na party ya kukutana na kufahamiana.
Tarehe 30 kutakuwa na ziara ya kutembelea Pearl Habour bandari
iliyoharibiwa na majeshi ya Japan mwaka 1941na kuifanya Marekani
ijiingize kwenye vita ya pili ya dunia.
Tarehe 31 ni siku rasmi ya
ufunguzi wa mkutano huo ambapo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa
Marekani ataufungua rasmi. Wajumbe wengine watakaohutubia ni pamoja na
Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
Mtanzania Onesmo Ngowi.
Wengine ni Lindsey Tucker ambaye
ni mwenyekiti wa Kamati ya Ubingwa wa IBF, William James ambaye ni
mwenyekiti wa Kamati ya Viwango wa IBF.
Nao Lou Priluka ambaye ni Katibu
wa bodi ya wakurugenzi wa IBF atazungumza pia. Aidha Al Maiyer ambaye ni
Mwakamu wa Rais wa IBF atazungumza. Ray Wheatler ambaye anaiwakilisha
IBF katika bara la Asia atazungumza.
Rarehe 1 Juni kutakuwa na semina
ya Utibabu pamona na Marefari. Tarehe 2 kutakuwa na semina ya Majaji
pamoja na programu maalum kwa IBF zitawakilishwa. Mkutano huu utafungwa
rasmi tarehe 2 Juni na Mstahiki Meya wa jiji la Honolulu.
Imetumwa toka Honolulu, Hawaii,
Marekani na;
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
President, Tanzania Professional
Boxing Commission(TPBC)
Director, Commonwealth (English
Empire) Boxing Council (CBC)
Coordinator, Moshi Sister Cities
Committee
Coordinator, International
Education and Resources Network (iEARN) to TANZANIA
No comments :
Post a Comment