Na Onesmo Ngowi
Masumbiwi
au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa,
mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni
kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini
kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha
nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana
kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa
endelea………………………………….!
Mabondia
wengi na walio mabingwa wa dunia huajiri "cutman" kwa kipindi chote cha
maisha yao ya ngumi. Kutokana na umuhimu wa kumhudumia bondia wake
vizuri ma-cutman wengi wanalipwa fedha zaidi ya madaktari katika
mpambano.
Katika
mpambano wa ngumi kuna washika vibao (Card Girls) vinaoonyesha raundi
inayofuata. Mara nyingi watu hawa huwa ni wasichana wanamitindo au
waliobobea kwenye majukwaa kama wanamuziki, wanamitindo, wacheza shoo
n.k. Kila raundi inapoisha mshika kibao huingia kwenye ulingo akitembea
kwa maringo na kuonyesha raundi inayofuata.
Mara
nyingi mwendo wake husaidiwa na musiki mororo unaopigwa na watazamaji
hufuatilia kwa makelele ya furaha. Wapo vile vile washika vibao ambao ni
wanaume wanaofanya mazoezi ya kutunisha musuli na haswa mpambano
wenyewe unapokuwa ni wa wanawake.
Vile
vile kuna mtangazaji (Commentator) ambaye anatakiwa kutangaza mpambano
wenyewe. Mtangazaji wa mpambano hutangaza mpambano wenyewe kwa ujumla
akianzia na aina ya mpambano, wageni waliohudhuria na mabondia wahusika.
Pengine
ni wakati anapotangaza mabondia husika ndipo anapotakiwa kutumia
madoido ya hali ya juu kumnadi kila bondia. Kazi yake nyingine ni
kutangaza matokeo ya kila mpambano haswa inapozingatiwa kuwa mchezo wa
ngumi unajumuisha mapambano mengi madogo madogo (supporting bouts) kabla
ya mpambano mkubwa.
Waliotajwa hapo juu ndio wahusika muhimu mbali na promota na meneja kuendesha pambano la ngumi.
MIFUMO YA NGUMI NA MADHARA YAKE KWENYE MAENDELEO YAKE
Mifumo
ya ngumi imekuwa inabadilika na wakati, tangu ngumi zilipoanza. Lakini
nitaanzia na hapa kwetu Tanzania. Ipo mifano mingi inayoonyesha namna
mabondia wetu wa kitanzania walivyo na uwezo mdogo wa maswala ya ngumi.
Mfano mmoja ni jinsi Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)
ilivyokwisha jitahidi kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili
kuwawezesha baadhi ya mabondia kushindania tuzo mbalimbali za kimataifa.
Kana
kwamba ni kazi ta TPBC kuhakikisha kwamba bondia bingwa wa tuzo hizi
kuzitetea, mabondia hawa wanaishia kupoteza mataji yote waliyoyashinda
kwa gharama kubwa na juhudi hizi za TPBC bila kuyatetea.
Baadhi
yao wakitumiwa na wababaishaji wachache wanaojiita mameneja feki
wanaodiriki hata kuushutumu uongozi wa TPBC kwamba uliuuza mikanda yao
ya ubingwa. Kuna usemi wa kiswahili unaosema kwamba “akutukanaye hakuchagulii tusi”. Ni kioja cha hali ya juu tena dhihaka isiyo na upeo kwa mtu kusema kwamba mkanda wake umeuzwa.
Mkanda
wa bondia ni mali yake na haiwezekani tu mtu akajitokeza barabarani
amevaa mkanda wa ubingwa asiokuwanao. Kufanya hivi ni sawa na mtu kuvaa
nguo za askari wa zima moto na kwenda nazo disko.
Dhihaka
kama hizi na nyingine nyingi zilnaufanya uongozi wa TPBC uachane na
kujishughulisha na maswala ya kupromoti na kumeneji. Kwa kuwa juhudi
zake za kuwasaidia mabondia pale ambapo mapromota na mameneja hawakuwepo
zinachukuliwa kama njia mbadala ya kujinufaisha kifedha, iliamua
kukoma.
Mikanda
ambayo TPBC iliigharamia ili kuhakikishia mabondia wa kitanzania
wanayashinda ni pamoja na IBF/Afrika, CBC, ECAPBF na WBU.
Ni
vizuri nieleze tu kwamba bondia anayeshinda mkanda wa ubingwa anatakiwa
awe ameutetea katika kipindi kati ya miezi minne na mwaka mmoja
(Division ndogo kuanzia Light Fly mpaka Super Light Weight wanatakiwa
wawe wametetea katika kipindi cha miezi sita, Kunzia Welterweight mpaka
Heavyweight anatakiwa awe ametetea katika kipindi cha mwaka mmoja husuan
ubingwa wa dunia). Mashirikisho mengi madogo mbali na IBF, WBA, WBO na
WBC hayana sheria ngumu zinazomtaka bondia atetee ubingwa wake katika
kipindi hiki kilichotajwa hapo juu.
Hivyo
huwapa muda kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja an wakati mwingine
bondi anakaa tu na mkanda mpaka atakapojitokeza bondia mwingne
anayeutaka.
Lakini
mashirikisho kama IBF, WBC, WBO na WBA ni lazima bondia bingwa acheze
na bondia anayemfuata kwenye viwango katika kipindi kilichotajwa cha
miezi sita kwa ubingwa wa bara (Continental) mpaka mabara
(Intercontinental).
Sheria
za mashirikisho haya zimeufanya mchezo wa ngumi kuwa na upinzani wa
hali ya juu. Bingwa anapotakiwa kutetea ubingwa na bondia anayemfuata
kwenye viwango na kwa muda uliotakiwa kunaufanya mchezo wa ngumi kuwa na
upinzani wa hali ya juu.
Bondia
anaposhindwa kutetea ubingwa wake katika kipindi hiki hunyanganywa
ubingwa na kutangazwa kuwa ubingwa wenyewe uko wazi. Ubingwa
uliotangazwa kuwa wazi unawafanya mabondia walio namba moja hadi nne
kucheza mapambano ya mtoano (Elimination Titles) ili kuwapata mabondia wawili watakaoshindania ubingwa.
Kwa
ajili ya upinzani na malipo mazuri mapambano yote ya mashirikisho haya
hutangazwa kwa njia ya tenda (bidding). Mapromota wanatakiwa watume ofa
ya fedha watakazolipa mabondia na atakayetoa donge nono ndiye
anayeshinda katika tenda ya kupromoti pambano husika.
Kwa
wenzetu inakuwa rahisi kwani mifumo yao wa kupromoti ngumi inamruhusu
promota kuweza kukubaliana na makampuni mbalimbali ya mitandao ya
televisheni itakayomlipa fedha za kupromoti. Anapopiga mahesabu yake na
kuona kuwa anazo fedha za kutosha na faida ndipo anapotuma tenda yake.
Iaendelea………………………….!
No comments :
Post a Comment