KIKOSI cha wachezaji 30 cha timu ya taifa ya
Zanzibar kimetangazwa na kocha mkuu wa timu hiyo Salum Bahusi bila ya jina la
nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Cannavaro na Aggrey Morris wa Azam FC.
Kwa mujibu wa habari kutoka Zanzibar, kikosi hicho
ambacho kinatarajiwa kushiriki Kombe la Chalenji kuanzia Novemba 27 mwaka huu
jijini Nairobi Kenya, Kocha wa Zanzibar Heroes, Bausi amesema kikosi hicho
kitaingia kambini Oktoba 27 mwaka huu na keshokutwa jumatano wachezaji wote
walioitwa kikosini watafanyiwa vipimo.
Katika kikosi kilichotajwa leo, MAKIPA ni Mwadini
Ali (Azam), Abdallah Rashidi (Ruvu Shooting), Ali Suleiman (KMKM).
MABEKI ni Mohamed Azan (Polisi), Waziri Salum
(Azam), Shafi Hassan (Malindi), Mohamed Faki (Zimamoto), Salum Haji (Miembeni),
Said Yussuf (Mtende), Mohamed Othman (Jamhuri), Mussa Said (Chwaka Stars), Nassor
Masoud ‘Chollo’ kutoka Simba.
VIUNGO ni Abdulhalim Humud (Simba), Sabri Ali (JKT
Oljoro), Adeyum Saleh (Simba), Isihaka Othman (JKU), Ali Kani (JKT Oljoro), Hamad
Mshamata (Chuoni), Suleiman Hamad (Miembeni), Awadh Juma na Masoud Ali wote wa
Mtibwa Sugar.
WASHAMBULIAJI ni Seif Karihe (Azam), Suleiman Kasim
Solembe (Coastal Union), Khamis Mcha (Azam), Amour Omary (Miembeni), Amir Hamad
(JKT Oljoro), Jaku Joma (Mafunzo), Faki Nahoda (Kimbunga), Hassan Seif (Mtibwa Sugar),
Juma Ali Yussuf wa New Generation.
No comments :
Post a Comment