Afisa Mwandamizi toka Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) Masozi Nyirenda akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar Es Salaam juu ya ufadhili wa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Sigara Tanzania
(TTC) kwa mafunzo ya kuongeza uwezo wa wanafunzi wa kike katika masomo ya
Sayansi, kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Misaada kwa
Jamii toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) Martha Saivoiye.
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe akielezea
mipango ya Mamlaka hiyo ya kuendelea kutafuta wafadhili zaidi ili kuongeza
idadi ya wanafunzi kike wanaosoma masomo ya Sayansi,katikati ni Afisa
Mwandamizi toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Masozi Nyirenda na kushoto ni
Meneja Mawsiliano na Misaada kwa Jamii toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC)
Martha Saivoiye.
Meneja Mawasiliano na Misaada kwa Jamii
toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) Martha Saivoiye akielezea mikakati ya Kampuni hiyo kuongeza
ufadhili ili kuwa na idadi ya
wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya Sayansi, katikati ni Afisa
Mwandamizi toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Masozi Nyirenda na kulia ni
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia
Lupembe
Mratibu wa kozi ya awali toka Taasisi ya
Teknolojia Dar Es Salaam(DIT) Mhadhiri Matara
Ryoba akielezea namna ya kupata wanafunzi na uendeshaji wa kozi, kulia Afisa
Habari toka Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.
No comments :
Post a Comment