Rais
Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi
akihutubia vijana mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya tusome
Tanzania (Let us read Tanzania) aliyoizindua leo katika viwanja vya
Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya vijana walioshiriki uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us
read Tanzania) wakifuatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe.
Benjamini William Mkapa (hayupo pichani) leo katika viwanja vya Makao
Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa wadau toka timu ya Let us read Tanzania akimpa maelezo juu ya vitabu
mbalimbali viliyotungwa na waandishi mashuhuri ndani na nje ya nchi.
Rais
Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi
akiwasomea hadithi mbalimbali na kuwauliza maswali mbalimbali watoto
ambao ni wanafunzi toka shule mmbalimbali leo katika viwanja vya Makao
Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
====== ======== =======
RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMINI WILLIAM MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA (LET US READ TANZANIA CAMPAIGN).
Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.
11/10/2013.
RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa amezindua rasmi Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s read Tanzania Campaign) iliyoandaliwa
na wadau mbalimbali nchini wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa
kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.
Katika
uzinduzi huo, Mhe. Mkapa ameipongeza kamati ya wadau waandaaji wa
kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika kuhakikisha kuwa watoto wa shule
ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea wenyewe na anatumaini kuwa
watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha yao.
“Tabia ya kusoma inamjenga mtu kifikra na kumpa mtu mtazamo”. Alisema Mhe. Mkapa. Mhe.
Mkapa ameongeza kuwa kwa kuwa elimu haina mwisho, kusoma ni namna ya
kujielimisha siku hadi siku na kufungua mambo mapya yanayoipa akili
changamoto, hivyo amewasisitizia vijana wajijengee utamaduni wa kusoma
hasa vitabu vya kiswahili na Kiingereza.
“Someni kazi za Shaabani Robert mwandishi mkongwe wa Tanzania, someni kazi za Mariam Abdallah, Ngugi wa Thio’ngo , Chinua Achebe, Ole Soyinka na .” Alisema Mhe. Mkapa.
Aidha, Mhe. Mkapa ametoarai kwa wadau waandalizi wa kampeni ya “Let’s read Tanzania Campaign” kuwa
zoezi hilo lisiishie hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na
haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu
hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya
ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.
Let’s
read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi
mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea
utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za
vijana na kuwasaidia katika maisha yao.
No comments :
Post a Comment