Beki wa Mtibwa Sugar, Paul Ngalema akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.
MABAO mawili ya Mrisho Ngassa na Didier Kavumbagu
yameiwezesha Yanga kuikaribia Simba wanaoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya
kufikia pointi 12 nyuma pointi tatu na vinara hao.
Yanga ambao walianza ligi hiyo kwa kususua
wamefanikiwa kuibakiribia Simba baada ya kuibua na ushindi huo dhidi ya Mtibwa
Sugara katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga ambao leo walikuwa uwanjani bila kiungo wao
Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na matatizo ya kifamilia, walianza kupata
bao la kwanza dakika ya sita kupitia kwa Ngassa kabla ya Kavumbagu kutupia bao
la pili dakika ya 24.
Katika mchezo mwingine uliochezwa jijini Tanga,
Mgambo walishindfwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kipigo
cha bao 1-0 dhidi ya Prisons mfungaji akiwa Peter Michael dakika ya 72.
Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza akilimiki mpira mbele ya beki wa Mtibwa, Hassan Ramadhani
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akiwajibika.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akifunga bao la pili katika mchezo huo, huku kipa wa Mtibwa, Hussein Ashiraf akigaagaa
Mrisho Ngassa akishangilia baada ya kufunga bao lake la kwanza toka alipojiunga na Yanga kwa mara ya pili.
No comments :
Post a Comment