Maandalizi ya mapambano ya ngumi
yanayotegemewa kufanyika katika ukumbi
wa ccm mwinjuma-mwananyamala ambayo
inawezekana yakavunja rekodi ya mapambano mengi kufanyika kwa mara moja kwa
mwaka huu kuliko mengine,kwani kuna zaidi ya mapambano 14 makali ya
utangulizi.hii itasaidia kwa wale watakaokuwa mpirani wa samba na yanga kuwahi
mapambano makubwa yatakayosalia ambayo
ni ya bondia mwenye ngumi za hatari na
mara nyingi huwazimisha wapinzani wake Zumba kukwe au chenji dola kama anavyojiita
mwenyewe wa kibaha atakae zipiga na Ali
boznia wa Tanga atakaefuatana na alan kamote na meneja wao ali mwanzoa
wakitokea mkoani tanga, mapambano mengine ni
Mwaite Juma na Shadrack ignas hii ni vita kali ya ulingoni wote sugu
wote wabishi kushindwa, nae bingwa wa zamani wa bantam Ajibu salum atapimana ubavu na Martin
Richard,huku mbena Rajab akizipiga na
Godwin Mawe, Ibrahim class na Rashid
Ali, Hassan kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim chuma na Shaban Manjoly,
mdogo wake francis miyeyusho Yona
miyeyusho atacheza na julias Thomas,
Abdalla ruwanje na Bakari zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa
mwananyamala sokoni joseph stanslaus(amita
au jose mawe) na mbabe wa manzese sokoni
shaban seif(body kitongoji) pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa
mabondia hawa, nae yasin omari atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na
mapambano mengine kadhaa ya vijana
wadogo wenye vipaji vya mchezo wa ngumi.
Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR(peche
boy) atakaezipiga na ATHONY MATHIAS katika pambano la round nane
na SADO PHILEMON ambae anategemewa kuwasili alhamis akitokea songea atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito
wa middle kutafuta mshindi wa
atakaezipiga na Thomas mashali katika pambano la ubingwa.kwa ufupi mabondia
wote wapo katika hali nzuri ya ushindani na wanategemea kupima afya zao na
uzito siku ya jumamosi saa nne asubuhi hapohapo katika ukumbi wa ccm mwinjuma
mwananyamala A
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
5 days ago
No comments :
Post a Comment