NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete msaada wa vyakula wenye
thamani ya Sh. milioni 5.5 kwa makundi maalum ambayo ni wazee na
wasiojiweza, watoto yatima na watoto walio katika mkinzano na kisheria
kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Edi El Hajj.
Msaada
huo ulitolewa leo kwa niaba ya Rais Kikwete , na Kaimu Kamishna wa
Usatawi wa Jamii Rabirira Mushi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye
mahabusu ya watoto iliyopo Regency jijini Dares Salaam kwa vituo na
makazi 12 ya makundi hayo yaliyopo hapa nchini.
“
Mhe. Rais ametoa zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia ili
kuona kwamba watoto na wazee hawa wanajumuika na wanajamii wengine
katika sherehe hii,” alisema Rabirira.
Alivitaja
vituo vilipokea msaada huo kuwa ni kituo cha watoto Dar Al arkam na
Nunge vyote viko(Temeke), Msongola Orphaned Centre(Ilala),
Furaha(Kinondoni) Mother Theresa(Mburahati), Malaika Kids
Home(Mkuranga) na makazi ya wazee na wasiojiweza cha Kilima(Bukoba
Vijijini).
Vituo
vingine ni Mahabusi ya watoto(Arusha Mjini), mahabusi ya watoto(Tanga
Mjini), makazi ya wazeee Mwanzange(Tanga), makao ya watoto Istikana
(Pemba ) na makazi ya wazee Sebuleni(Unguja).
Akizungumzia
kuhusu msaada huo kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa kituo cha Msongola
Orphaned Trust Fund, Shanta Deus alimshukuru Rais Kikwete kwa moyo
wake wa kujitolea kwa makundi hayo huku akiwataka watu wengine kuiga
mfano.
“Ninawaomba
watu wengine, sekta binfasi na kampuni mbalimbali kuiga mfano huu ili
kuweza kuwasaidia watoto yatima na wanaoshi katika mazingira hatarishi
pamoja na makundi maalum kwa kutoa misaada mbalimbali,”alisisitiza
Shanta.
Naye
Sista Oliver Paulo ambaye ni mlezi wa makao ya watoto ya yatima,
kijiji cha Furaha aliishauri jamii iwe tabia ya kushirikiana na makundi
hayo katika sherehe mbalimbali na kuwasaidia.
No comments :
Post a Comment